UWT BUKOMBE YAJIPANGA KUTEKETEZA UPINZANI UCHAGUZI MKUU WA SERIKALI ZA VIJIJI NA VITONGOJI MWAKA 2024

Na Zena seleman

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa uwt wilaya ya Bukombe Juliet Simon wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya uwt wilaya ya Bukombe katika kata ya Bukombe wakati wakikagua uhai  wa jumuiya na maendeleo ya chama.

Juliet amewataka wanawake wa uwt kujitokeza katika kugombea  nyazifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaaa na vitongoji na kujitokeza katika kuhakiki daftari la kudumu la mpiga kura 

"Niwaombe kina mama tujitokeze katika kugombea uchaguzi mkuu wa serikali za mitaaa na vitongoji kupitia chama Cha mapinduzi ccm ikiwa lengo la kumuunga mkono mhe. Rais wa Jumhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu wa serikali mwaka 2025 "alisema Juliet


Katibu wa uwt  wilaya ya Bukombe Teddy  Mageni kwa upande wake amewataka viongozi wa kata na matawi  kuacha tabia ya majungu na wafanye kazi ili kuleta tija kuanzia ngazi ya tawi kata, wilaya na Taifa kwa ujumla .

 " Niwaombe viongozi wenzangu tufanye kazi kwa kushirikiana na kueshimiana  ili tuweze kukijenga chama chetu kwa kuepuka majungu na migogoro"alisema mageni.

Awali Diwani wa kata ya Bukombe Rozaria Masokola amewashukuru viongozi wa uwt wa wilaya ya Bukombe kwa kuendelea kufanya kazi kwa kukagua uhai wa chama na jumuiya zake na kuhamasisha wanawake kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaaa na vitongoji.

"Niwashukuru Sana viongozi wetu wa wilaya kwa kuendelea kuhamasisha katika kuelekea uchaguzi mkuu wa serikali za mitaaa na vitongoji  hivyo mim Kama diwani wa kata ya Bukombe nitahakikisha Bukombe inachukua vijiji na vitongoji vyote kupitia chama chetu Cha mapinduzi ccm."alisema Masokolo.

Awali ya yote kamati ya utekelezaji ya uwt wilaya ya Bukombe wamefanya ziara katika kata tatu ikiwemo kata ya Bukombe,kata ya Lyambamgongo, pamoja na kata ya ushirombo.

Comments