NISHATI SAFI YA KUPIKIA ITALETA MANUFAA KATIKA JAMII- DKT TULIA

  Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge duniani, Dkt. Tulia Ackson amesema nishati safi ya kupikia italeta manufaa makubwa katika jamii hasa kwa wanawake kwani pia itawakomboa kiuchumi.


Dkt. Tulia amesema hayo leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam ambapo kumefanyika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 - 2034.


Dkt. Tulia amefafanua kwamba wanawake ndio watumiaji wakubwa wa nishati chafu ya kupikia kama mkaa na kuni hivyo wanatumia muda mrefu kwenda kutafuta nishati hizo na kusababisha shughuli za maendeleo kusimama.


Aidha Dkt. Tulia amesema tayari Bunge limepitisha bajeti ya nishati safi ya kupikia ili wananchi waweze kufikiwa nayo kwa urahisi.

Comments