MWENYEKITI UWT AHIMIZA MSHIKAMANO

 

Na, Zena Seleman 

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Bukombe morning Geita Juliet Simon amewaomba wanawake wa jumuia kushikamana kwa pamoja ili kuendelea kutafuta wanachama wapya.

Wito huo aliutoa wakati akikabizi kadi 162 kwa wanachama wapya wa UWT waliyo jitokeza kwenye ziara walipofika kata ya Namonge. 

Kwenye ziara hiyo aliambatana na wajumbe wa kamati ya utekelezaji UWT Wilaya ya Bukombe kwa lengo la kwenda wanahamasisha wanawake kujiunga na UWT  na kukagua uhai wa jumuiya na Chama.

" Leo tumekabidhi kadi kwa wanachama wapya 162 waliojitokeza katika kata ya namonge, ampapo ziara yetu ni kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika kuhakikisha daftari la kudumu la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za  mtaa zinafanikiwa vyema mwaka huu", Alisema Juliet. 

Katibuwa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy Mageni alitumia ziara hiyo kwenda anamshukuru mbunge wa jimbo la BUKOMBE, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko kwa kuendelea kuleta maendeleo katika Wilaya  hali ambayo inapelekea hali ya kisiasa kuwa tulivu  katika kila kata.

"Nipende kumshukuru Sana Mbunge wetu Dkt. Biteko kwa kuendelea kuwa kiongozi Bora na mahili kila iitwapo leo na amekuwa mfano wa kuigwa kwa hata sisi viongozi wengine hivyo nipende kuwaomba wajumbe lakini ni viongozi katika mkutano huu tuige mfano mzuri kwa mbunge wetu ili tuendelee kuilinda irani ya chama chetu Cha mapinduzi kwa maendeleo ya kuanzia kitogoji Hadi Wilaya na Taifa kwa ujumla", alisema Teddy. 

Mariam Meshack ni mmoja wa wanawake aliechukua kadi na kujiunga na jumuiya ya UWT katika kata ya Namonge ali ishukuru Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutokana na utendaji mzuri wa kazi na kuleta maendeleo. 

Meshaki alisema Rais Samia kila Mkoa amepeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambayo imenifanya kujiunga na UWT kufatia uchapakazi wake sisi wanawake tutaendelea kuunga mkono kazi zinazo fanywa na Chama na S Serikali.


Comments