ENDELEENI KUSHIRIKI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO-DC MURAGILI



  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Eng. Paskasi Muragili amewataka Wananchi wa Kata ya Katome kuendelea kushiriki katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

  Muragili ameyasema hayo tarehe 16 April 2024 alipokuwa anazungumza na Wananchi wa Kata ya Katome wakati wa Ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi na kukagua Miradi ya Maendeleo katika kata hiyo.



    Wakati wa Ziara hiyo Mhe. Muragili ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Katome iliyopo katika kijiji cha Miyenze ambayo imejengwa kwa nguvu za Wananchi ambapo hadi sasa ujenzi huo umegharimu kiasi cha Shilingi 13,946,000/=

     “Hongereni sana Wananchi wa Kata ya Katome na endeleeni kushiriki nguvu kazi katika ujenzi wa Miradi kwa ajili ya Maendeleo yenu”

   Vilevile Muragili alitembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa barabara ya Ntagalo-Kona 4-Miyenze yenye urefu wa kilomita 6.90 na barabara ya Miyenze-Butinzya yenye urefu wa Kilomita 6.31 na ujenzi wa kalvati laini 8 kwenye barabara ya Ntagalo-Kona 4-Miyenze na kalvati laini 18 kwenye barabara ya Miyenze-Butinzya.



    Aidha Muragili amemtaka muhandisi wa TARURA kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kwa wakati ili kupunguza adha kwa wananchi katika kusafirisha mazao yao.

     “Ongezeni kasi katika ujenzi wa barabara hii ili ikamilike kwa wakati uliokusudiwa”



      Kwa upande wake diwani wa Kata ya Katome Mhe. Joseph Maganga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo Kwani imefungua shughuli za maendeleo kiuchumi.




      Katika Ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Kata mbalimbali za Wilaya ya Bukombe.

Comments