SIMBA NA YANGA ZAPANDA VIWANGO CAF, ZAWEKA REKODI MPYA BARANI AFRICA

 


Timu za Soka za Tanzania Simba na Yanga zimepanda Viwango kwa mujibu wa Mfumo Rasmi wa Daraja na Alama wa CAF kwa kipindi cha Miaka Mitano(5) yaani CAF 5 YEARS RANKING SYSTEM baada ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imepanda hadi nafasi ya 5 wakifikisha alama 39 kutoka nafasi ya 9 wakiwa na Alama 35 Msimu uliopita huku Yanga wakichumpa hadi nafasi ya 12 wakifikisha alama 31 kutoka nafasi ya 18 wakiwa na Alama 20 Msimu uliopita.

Mfumo huu hutoa alama 3 ukifuzu Robo Fainali, Alama 4 ukifuzu Nusu Fainali na Alama 5 na 6 Ukifika Fainali huku Bingwa akichukua Alama 6 na Mshindi wa pili Alama 5 kwa Upande wa Ligi ya Mabingwa.

Upande wa Kombe la Shirikisho, Alama 2 kwa Robo Fainali, Alama 3 kwa Nusu Fainali, Alama 4 na 5 kwa Wanafainali huku Bingwa akichukua alama 5 na mshindi wa pili Alama 4.

Kila baada ya Msimu Mmoja kumalizika, huondolewa msimu mmoja kwenye mahesabu ili kuongezeka mwaka mmoja wa Msimu ujao, ndivyo mfumo unavyofanya kazi.

Aidha Shirikisho la Soka la Tanzania limeendelea Kushika nafasi ya 6 huku bado pakiwa na nafasi ya kupanda zaidi kama vilabu vya Tanzania, Simba na Yanga wataendelea kufanya vema msimu huu.

Katika Upande Mwingine, Tanzania ndio taifa pekee ambalo limeingiza Timu 2 kwenye hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa CAF msimu huu huku Mataifa yaliyobaki yakiingiza timu 1 pekee.

Kwa mara ya kwanza kwenye Historia ya Soka la Tanzania, Simba na Yanga zatinga Robo Fainali ya michuano hii kwa pamoja.

Comments