WANANCHI TUMIENI MAJI SAFI YANAYOZALISHWA NA MAMLAKA ZA MAJI KUJIEPUSHA NA MAGOJWA YA MLIPUKO.


 Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Said Nkumba amewataka wakazi wa wilaya hiyo  kutumia zaidi maji yanayozalishwa na Mamlaka za maji ikiwemo RUWASA  kwa lengo la kujiepusha na mlipuko wa magojwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu kinachosababishwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.


Nkumba amebainisha hayo wakati akifungua kikao kazi cha robo ya pili ya mwaka cha Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Geita kilichofanyika wilayani Bukombe amesema wanachi wengi licha ya kuwepo kwa miradi ya maji wamekuwa wakiendelea na matumizi ya maji ya visima vifupi ambayo siyo safi na salama hivyo ni vyema kutumia maji katika mamlaka za maji ambayo yametibiwa kitalamu ili kujiepusha na magojwa ya mlipuko.


DC Nkumba ametumia nafasi hiyo kukabidhi pikipiki tatu kwa watumishi wa RUWASA Wilaya ya Bukombo na wakati akikabidhi pikipiki amewataka watumishi hao kuzitumia kuleta huduma chanya kwa wananchi na si vinginevyo na kuzitunza vizuri ili zitumike kwa mda mrefu.



Meneja wa RUWASA Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amesema kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji vijijini katika Mkoa wa Geita imefikia asilimia 55 na mpaka kufukia Disemba 2024 hali ya upatikanaji wa maji itakuwa asilimia 74 huku Mkoa huo umetengewa zaidi ya bilioni 24 kwa mwaka wa fedha 2023/24  ili kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji vijijini kwa lengo la kufikia adhima ya serikali ya kumtua ndo mama kichwani katika kila maeneo.


Nao baadhi ya viongozi katika Jumuia za watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWS’o)  katika wilaya ya bukombe wameishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki hizo na kwamba zinakwenda kumaliza changamoto za ukosefu wa usafiri na sasa utendaji kazi unakwenda kuongezeka zaidi hasa ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Comments