M/K WA CCM MKOA WA GEITA AIPONGEZA BUKOMBE, UPINZANI WA PUPUTIKA, WANACHAMA ZAIDI YA 200 WAREJESHA KADI BUKOMBE

  


Ametoa pongezi hizo  mwenyekiti wa Mkoa wa geita Nicholas kasendamila wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama katika kata ya ushirombo wilayani Bukombe mkoani geita.


Kasendamila aliipongeza  wilaya ya Bukombe kwa mwenendo mzuri na Hali nzuri ya kisiasa kutokana na  watu zaidi kuendelea kurudi ndani ya chama 


"Niwapongeze Sana viongozi wa chama wa wilaya ya Bukombe kwa kazi nzuri mnayoifanya sisi Kama viongozi wa Mkoa tunafarijika Sana kutokana na Hali ya kisiasa ndani ya wilaya hii kasendamila alisema"


Hata hivyo kasendamila aligawa bendara  za chama Cha mapinduzi zaidi ya 100 kwa mabarozi wa kata ya ushirombo  na kuwataka kufanya siasa zenye afya katika jamii


Naye  diwani wa kata hiyo lameck walangi alimshukuru mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto biteko kwa kuwa muwakirishi mzuri bungeni na kusababisha raisi Samia kumwaga fedha za miradi ya maendeleo katika Jimbo la Bukombe 


"Napenda nimshukuru Sana mbunge wetu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwa msemaji mzuri na kusababisha Jimbo lake kuletewa fedha za maendeleo na raisi wetu  walangi alisema"


Naye mwenyewe kiti wa CCM wilaya ya Bukombe Matondo kihanda  ameowaomba viongozi wa ngazi tofauti ndani ya chama kuweza kushirikiana kwa pamoja kuepuka migogoro  ili kuweza kufanya kazi na kuleta maendeleo  katiaka jamii   Huku akimshukuru raisi Samia kwa kuichagua Bukombe kuiletea fedha za maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya afya,elimu,kilimo , barabara na umeme.


" Nipende kutoa shukurani zangu za dhati kwa raisi wetu Samia suluhu Hassan kwa kuichagua wilaya yetu ya Bukombe  huku akimpongeza mbunge wa Jimbo la Bukombe dkt.Biteko kwa kazi nzuri anazozifanya hakika Bukombe ni kusema na kutenda  alisema kihanda."

Comments