MADIWAN MBOGWE WAAHIDI KUHAMASISHA UJENZI WA VYOO BORA

 


MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wameahidi kuhamasisha wanachi kujenga vyoo Bora kwenye familia zao ili kunufaika halmashau kiuchumi katika miradi ya maendeleo na kujikinga na maginjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Hayo aliyasema Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbigwe Viseti Businga kwenye semina ya siku moja ili yo kuwa imeadaliwa na afisa afya wikaya ya Mbigwe.

Awali Afisa afya Wilaya ya Mbogwe Pendael Mazengo wakati akitoa  mafunzo na faida ya jamii inapo jenga vyoo bora wananchi uepuka kupata maginjwa ya milipuko na halmashauri itapokea fedha nyingi za miradi.

Mazengo alisema kapeni za kuhamasisha ujenzi wa vyo bora Wilayani humo walianza mwaka 2019/2020 hadi kufikia 2023/2024 naaza ya wananchi kujenga vyoo bora halmashauri imepokea shilingi 3 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo miradi 30 katika kata 16 kati ya 17.

Alisema miradi hiyo inayotekelezwa kupitia mango huo wa matokeo ya kuhamasisha wananchi kujenga vyoo ni ujenzi wa vyoo, visima virefu na vichomea taka kwenye vituo vya afaya  na Zahanati, Hospital ,shule na stendi ya mabasi.

Mazengo kupitia semina hiyo aliwaeleza madiwani kuwa kutokana na ofisi ya Afisa afya kutoa Elimu kwa wananchi hadi sasa zaidi ya kaya Elf 60 zimejenga vyoo bira ambavyo sio vya ghalama kubwa.

Kaimu mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbigwe Dkt. Zakayo Sungura akizungumza kwenye semina hiyo aliwaomba madiwani kusimamia Mira ya maedeleo ambayo inaletewa fedha na Serikali kupitia mpango wa kuhamasisha wananchi wajenge vyoo bora na kwamba tatuna kipindupindu kwenye Wilaya na Mkoa wa Geita.

"Madiwani simamieni fedha zinazoletwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni matokeo ya wanachi kuendelea kujenga vyoo  bora ijulikane kwamba Wilaya ya Mbogwe hadi Mkoa mzima having kipindupindu pindu ila madiwani tumiene lugha ya wananchi wajenge vyoo ili kueouka maginjwa ya mlipuko.

Mwenyekiti wa halmashauri Busiga akimpongeza Afisa afya Wilaya kwa kuiigizia halmashauri fedha kupitia Elimu aliyoifanya kwa wananchi uhuhimu wa vyoo.


Businga kupitia Semina hiyo aliwaomba madiwani kusimamia miradi inayoletwa  kwenye kata zao kwa kutambua kuwa zipo chini ya usimamizi wa madiwani wakishirikiana na viongozi wengine.



Comments