DKT.BITEKO ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA WASHIRIKI WA MICHEZO YA UMISETA NA UMITASHUMITA

 


Bukombe



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe ametoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA kwa mwaka 2024 kuanzia ngazi ya shule hadi Wilaya ili timu hizo ziweze kufanya vizuri na hatimaye ziweze kupata wachezaji bora na wenye vipaji ambao wataunganishwa kwenye timu ya Mkoa.


Vifaa hivyo amevikabidhi Afisa Michezo Wilaya Bi.Jenifa Kisusi kwa niaba ya Mhe. Mbunge kwa Walimu wa Michezo wa shule za Msingi na Sekondari kwa timu zinazoshiriki mashindano hayo.


Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Bi. Kisusi amemshukuru Mhe. Biteko kwa kuinua michezo katika wilaya ya Bukombe.

" Tunakushukuru sana Mhe.Biteko kwa kutupatia vifaa vya hivi. Tunatambua na kuthamini mchango wako wa kuendeleza michezo katika Wilaya yetu ya Bukombe."


Aidha Bi. JenifaKisusi amemuhakikishia Mhe.Mbunge kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imejipanga kuhakikisha inafanya mapinduzi makubwa katika mashindano kwasababu wameanza maandalizi mapema.


"Ninauhakika tutafanya vizuri katika mashindano kwani vifaa hivi ni sehemu ya Maandalizi yetu na tayari walimu wote wameishapewa maelekezo.








Comments

  1. Asante sana mh Mbunge na pia afisa michezo wetu Mungu awajalie maisha marefu🙏

    ReplyDelete

Post a Comment