BUKOMBE YAPOKEA MILIONI 658 KWA AJILI YA DAWA NA VIFAA TIBA


 Na,  zena Seleman, Bukombe

Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela wakati kamati  ya siasa Mkoa ikikagua miradi ya maendeleo inayo letewa fedha na Serikali wilayani Bukombe Mkoani Geita

Shigela alisema upande wa afya Rais Samia ameleta  fedha shilingi 658 milioni kwa ajili ya dawa na vifaa tiba huku shilingi 500 milioni zimeletwa  kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.

Alisema  upande wa barabara  zimetolewa shilingi 74 milioni zilizotokana na mfuko wa Jimbo hivyo aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko  kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya marekebisho ya barabara.

Shigela alisema  upande wa maji Serikali ilileta fedha na kuchimba visima 25 vyenye  thamani ya shilingi 80 milioni visima hivyo vinatarajia kuhudumia watu 100000  hivyo shida ya maji inaenda kutoweka kutokana na Rais Samia kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo alisema Shigela.


Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila wakati akikagua miradi hiyo ameipongeza wilaya ya Bukombe na viongozi wake kwa jitihada wanazo zifanya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kasendamila amewataka Wilaya zingine kuiga mfano  kutoka Wilaya ya Bukombe kwa kazi nzuri wanazo fanya kwa kushirikiana na viongozi wote huku akimshukuru Rais Samia  kwa kuichagua Bukombe na kuiletea fedha za miradi ya maendeleo.

Wananchi wa Wilaya ya Bukombe wakizungumza na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti Zainabu Mnubi alitoa shukurani kwa Serikali na Mbunge kwa kuendelea kutatua changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili. 

"Kwakweli zamani tulikuwa tunateseka Sana wanawake tukitaka kujifungua hospital zilikuwa mbali ukilinganisha na barabara zilikuwa mbovu Ila hivi Sasa tunaishukuru Sana Serikali kwa na Mbunge wetu Dkt. Doto Biteko kutuona watu wa Bukombe", alisema Mnubi. 
 
Elizabeth Gamaka ni miongoni mwa wananchi walio ishukuru Serikali yeye alisema zamani vifo vya mama na mtoto vilikuwa vingi sana kutokana na uhaba wa zahanati hivyo kupelekea wagonjwa kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma kwa uharaka zaidi Ila kwa sasaivi tunaishukuru Serikali kwa kutujengea zahanati na kusababisha kupunguza vifo. 

MWISHO

Comments