AFISA ARIDHI ANUSURIKA KUSHUSHWA CHEO MBOGWE

 


Afisa aridhi na maendeleo ya makazi Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita Manace Nkuli  anusurika  kushushwa cheo na madiwani wa halmashauri ya Wilaya hiyo baaya kuchachamaa kwenye Baraza la madiwani na kutaka afisa aridhi huyo ashushwe cheo kutokana na kufanya kazi kwa uzembe huku wananchi wakijenga bila kupimia viwanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri  ya Mbogwe Viceti Busiga alisema afisa huyo ameshindea kukusanya ushuru wa upimaji wa viwanja ambapo alitakiwa akusanye shilingi 16 milioni pia ada ya maombi ya viwanja alitakiwa kukusanya shilingi 5 milioni na ushuru wa mauzo ya viwanja alitakiwa kukusanya milioni 30  lakini hakuna mapato yoyote yalioyo kusanywa Hadi leo haliambayo inaonekana hatoshi.

Diwani viti maalumu Salome Sendeu alisema afisa ardhi hatoshi anasitaili kushushwa cheo ili awekwe mwingine kwenye nafasi hiyo ili viwanja vipimwi na halmashauri ipate mapato.

"lakini ikumbukwe ng'ombe hanenepeshwi siku ya mnada kwasaabu tumeongea sana muda mrefu leo hii hatuwezi kupata kitu chochote hivyo muda mwingine sheria isimame kama kushushwa cheo ashushwe tu mambo mengine yaendelee", alisema Sendeu.

Naye ambae ni diwani viti maalumu Pili Meshack  alipinga home hiyo na kuliomba baraza la madiwani kwa kumtetea afisa aridhi huyo.

Meshack aliitaka halmashauri kumuwezesha kumpa gari na mafuta ili aweze kufanya kazi ya upimaji viwanja na kukusanya mapato ya halmashauri hiyo  ndani ya mwezi mmoja.

Akijitetea kwenye baraza hilo asishushwe cheo afisa aridhi na maendelo ya makazi Nkuli aliliomba baraza la madiwani kumpa mda wa kutekeleza na kwamba atayafanyia kazi m azimio ya upimaji viwanja licha ya wasaidizi wake kunawakati hawamuelewi anacho kuelekeza.

Kaimu mkurungezi wa halmashauri ya  Lawi Musaki aliwaomba madiwani kumpa muda wa mwezi mmoja afisa aridhi afanye kazi ikishindikana hapo ichukuliwe hatua.

Katibu tawala wa Wilaya ya Mbogwe Jacob Rombo aliunga hoja ya m kurugenzi mtendaji na kwamba ofisi take Italian mafuta lita 150 ili afisa aridhi aede kupima viwanja na kukusanya mapato ya Serikali ndani ya mwezi mmoja.

"Nawaombeni madiwani kama itawapendeza nisimamenae mwezi mmoja kwa kukutana na wasaidizi wake wote na baada ya mwezi mmoja ikishindikana kutekeleza Monaco taka afanye nitakuwa wa kwanza kusema afisa aridhi ashughulikiwe kwa hatua Saudi", alisema Rombo.

Akifunga kikao Businga alisema maazimio ya baraza ilikuwa kushushwa cheo ila kwa maombi yaliyo tolewa na m kurugenzi na afisa hawala baraza tuna toa huo mwezi mmoja.


Comments