TIMU YA RIADHA YA BUNGE IMEENDELEA KUFANYA KUTIKISA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI



 Timu ya riadha ya Bunge Sports Club imeendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya 13 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Katika mbio zilizofanyika Desemba 16, 2023 kwenye Uwanja wa Bugesera Jijini Kigali nchini Rwanda, wabunge wa Tanzania waling’aa kwenye mbio za urefu mbalimbali.


Mbunge Anatropia Theonest aliongoza kwenye mbio za mita 800 wanawake, huku Mbunge Simai Hassan Sadiki ameshika nafasi ya kwanza upande wa wanaume.



Kwa upande wa mita 200, Nancy Nyalusi ameshika nafasi ya tatu kwa wanawake na Flatei Massay nafasi ya tatu kwa wanaume.


Aidha, katika mita 1600 wanawake kutembea kwa haraka, Regina Qwaray ameshika nafasi ya pili.


Katika mbio za mita 200 watumishi wanawake, Rai Kalinga ameshika nafasi ya kwanza na Suzana Audiface nafasi ya tatu.


Vile vile, katika mbio za kupokezana vijiti mita 400 watumishi wanawake walishika nafasi ya pili.


Takribani Mabunge ya nchi sita yanashiriki michezo hii ambayo ni Rwanda mwenyeji, Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Sudan Kusini.


Huku kauli mbiu ya mwaka huu ni maendeleo, amani kwa jumuiya yote ya Afrika Mashariki.



Comments