SIMBA BADO INACHECHEMEA, YALAZIMISHWA SARE YA 1-1





Simba imeshindwa kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo baada ya kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya Namungo FC ikiwa ni siku chache tangu ilipopoteza dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara


Mfungaji wa goli la Namungo ni Reliants Lusajo wakati Jean Baleke akafunga kwa upande wa Simba


Simba imefikisha pointi 19 katika michezo 8 ikiwa sawa na Azam FC yenye michezo 9 huku Yanga ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 24 katika michezo 9.

Comments