KUWENI NA MASHAMBA DARASA YA MFANO - DC NKUMBA





Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba amewataka Viongozi wote ndani ya Wilaya ya Bukombe kuhakikisha wanakuwa na mashamba darasa ili kutoa hamasa kwa wakulima.


"Katika Msimu huu wa Kilimo hakikisheni mnakuwa na mashamba darasa ili tuwe mfano bora kwa wananchi."


Aidha aliendelea kusema kuwa

" Hatuwezi kuwahamasisha wananchi kulima wakati sisi viongozi hatuna hata hekali moja inayoonyesha shughuli za kilimo."


Nkumba ameyasema hayo tarehe 20 Novemba, 2023 wakati alipotembelea mradi wa kilimo cha kisasa cha Mahindi katika kata ya  Bugelenga kitongoji cha Mwamboku.


Aidha amewata wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ili waweze kupata mazao mengi ambayo yatawasaidia katika kuwaletea maendeleo.


Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Zedekiah Solomon  amesema ili mkulima aweze kupata mavuno mazuri lazima aweze kupanda mapema, kupalili kwa wakati, kuhakikisha anakuwa na matumizi sahihi ya mbolea na namna bora ya kudhibiti visumbufu vya mmea.


Juma Mwanzilwa ambaye  ni mmiliki wa mradi wa kilimo cha kisasa cha Mahindi ameishukuru Divisheni ya Kilimo kwa kumtembelea  pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora ili aweze kupata mavuno mazuri na yenye tija.

Comments