EWURA YAPIGA MARUFUKU BIASHARA HOLELA YA MAFUTA

 



Na Ernest Magashi, Geita



Mbogwe. Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji kuanza kuzibiti biashara holela ya mafuta ili kulinda ubora wa mafuta usalama wa wananchi majanga ya milipuko ambayo inaweza kutokea wakati wa biashara hizo zikifanyika.


Hayo yameelezwa na meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA kada ya ziwa George Mhina wakati wa kikao cha kutoa Elimu kwa Umma kuhusiana na kazi na wajibu wa Ewura na kudhibiti biashara ya mafuta holela kilicho fanyika Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na kuhudhuriwa na wenyeviti wa Serikali za vijiji na kata hadi halmashauri.


Mhina wakati akitoa Elimu kuhusu kazi na wajibu wa Ewura sambamba na Elimu ya nishati ya mafuta alisema wilaya ya Mbogwe inaongoza kufanya biashara ya mafuta holela marufu kupiga nyoka kwenye magari kwa kanda ya ziwa haliambayo nikosa kisheria na nihatari kwa wananchi wanao ishi kwenye maeneo zinapo fanyika biashara hizo.


Alisema biashara hizo holela zinafanyika barabara kuu kutoka Kahama kuazia kata ya Bukandwe Wilaya ya Mbogwe hadi Ushirombo Wilaya ya Bukombe mbaya zaidi wakimaliza kupiga nyoka wanahifadhi mafuta kwenye madumu wanaficha kwenye makazi ya watu haliambayo ni hatari.


"Ewura tumeaza kwa kutoa Elimu hii nyinyi viongozi wa vijiji na kata zenye biashara hizo wambieni vijana wafanye biashara zingine kabla ya kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola wajuwe nikosa kisheria kunafaini au jela au vyote kwa pamoja nawaombeni madiwani wenyeviti wa vijiji haovijana waache hizo biashara nikero hasa kwa Serikali pia mafutahayo hayana ubira na hawalipi kodi ya Serikali", alisema Mhina.


Meneja huyo aliwaomba wananchi kuchagamkia frusa ya kuuza mafuta kwa kuomba leseni ikiwa kwa kanda ya ziwa EWURA imetoa leseni 575 na kati ya leseni hizo 26 wamiliki wamepewa barua za kujieleza ndani ya siku saba baada ya kubainika hawatoi huduma.


Ofisa biashara Wilaya Mbogwe Nyaruga Jeradi alipongeza EWURA kwa kufika na kutoa Elimu hiyo na kwamba kupitia Elimu hiyo viongozi wa Serikali za vijiji kuhakikisha wanafikisha elimu kwenye jamii kabla ya hatua zingine kuchukuliwa kwa wanao fanya biashara hizo.


Mwenyekiti wa kijiji cha Luhala Martha Masunga alisema nikweli biashara hizo zipo isipokuwa walikuwa hawajuwi madhara na hatari ambayo inaweza kutokea kutokana na elimu hii kwaza vijana wako hatarini kisheri nakwamba inatakiwa wapewe maelekezo ya kuacha na sio kwenda kuwabembeleza .


Diwani wa kata ya Lugunga Enoka Magulu aliwaomba viongozi na madiwani wezake ambao wamefika kwenye kikao hicho kuhakikisha wanafikisha ujumbe wa ewura kwa wahusika ili kukomesha biashara holela ya mafuta badalayake waombe leseni ili wafanye biashara kisheria.


MWISHO

Comments