Geita. Rais Samia Suluhu Hassan amempigia simu Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko na kuzungumza na walimu zaidi ya 2000 waliohudhuria maadhimisho ya siku ya walimu duniani yaliyofanyika katika uwanja wa shuke ya sekondari Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita na kuahidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenywe sekta ya elimu ma kuendelea kufanyia kazi changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya walimu kote nchini.
Akizungumza na walimu wa wilaya ya Bukombe kwa simu ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko kutokea nchini Qatar alikokwenda kwa shughuli za kiserikali Rais Samia amesema ataendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili walimu.
"Nawatia moyo mfanye maadhimisho yenu vizuri muwe na maazimio mazuri nammpe Naibu Waziri Mkuu tuje tuyafanyie kazi walimu ni jeshi kubwa niko Qatar nikitoka naeda Idia kutafuta ili nije tujenge nchi yetu serikali ipo tayari kusikiliza kero zenu na kuzifanyia kazi.
"Nimeanza kufanyia kazi changamoto kwenye sekta ya elimu na tutaendelea kuziondosha kidogo kidogo mpaka tufike mahali ambapo sio pakuridhisha kabisa lakini angalau hali iwe nzuri mazingira ya kufundishia yawe mazuri.
Rais Samia amesema yuko nchini Qatar na akitoka ataenda nchini India lengo likiwa ni kutafuta fursa(neema) na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maisha bora na kuwaomba walimu kumuombea arudi na mafanikio ili aje kuijenga nchi.
Rasi Samia amewataka walimu waliopo kwenye maadhimisho hayo kumueleza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati changamoto zao na mambo watakayokubaliana ili serikali iweze kuyatekeleza.
" Walimu ni jeshi kubwa na Serikali inathamini mchango mkubwa mnaoutoa, Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zenu ili hali zenu ziwe bora zaidi, hivyo nimemwagiza Naibu Waziri Mkuu, Mhe, Dkt Doto Biteko awasikilize kisha aniletee maazimio mliyoyafikia ili niyafanyie kazi" alisema Rais Samia.
Waziri Mkuu Mstafu Mizengo Pinda ambae alikuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya walimu dunia kiwilaya yaliyofanyika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita katika viwanja vya shule ya Ushirombo Sekondari Oktoba 6,2023 aliwaomba walimu kuendelea kutimiza wajibu wa kufundisha wakati Swrikali ikishughulikia changamoto zao licha ya zingine zimesha shughukikiwa ikiwemo kupandishwa madaraja.
Pinda amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imechukua jitihada mbalimbali ili kuboresha Sekta ya Elimu nchini.
Ametaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kukarabati na kujenga shule mpya ili kukidhi ongezeko la wanafunzi kutokana na mafanikio ya Sera ya Elimu bure ambapo katika mwaka 2022/2023 jumla ya shule mpya 873 zimejengwa.
Pia, ameeleza kuwa, ili kuhakikisha mtoto wa kike anafanya vyema katika masomo ya Sayansi na hisabati, Serikali inaendelea na ujenzi wa shule 26 za kitaifa kwa kila Mkoa ambapo shule 10 zimekamilika na zimeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha Tano.
Waziri Mkuu msitafu Mizengo Pinda amempongeza, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko kwa kuonesha kwa vitendo jinsi anavyowajali Walimu na kuwaheshimisha na kueleza kuwa, Walimu hao wanapata faraja kuona kuwa kuna kiongozi anatambua nafasi yao katika jamii katika kujenga nchi na kuwaasa Wabunge wengine kuiga mfano huo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe,
amewaasa wadau wa sekta ya Elimu kuthamini mchango unaotolewa na walimu na kazi kubwa wanayoifanya kwa jamii.
Waziri Dk Biteko ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akikabidhi tuzo maalum kwa walimu waliotoa mchango mkubwa kwenye maisha yake wakati wa safari yake ya kuwa Mwalimu pamoja na Walimu waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufaulishaji mzuri wa wanafunzi katika masomo kama ya Sayansi na uraia, ubunifu na utunzaji bora wa mazingira.
Dk Biteko ameongeza kuwa, Walimu ndio wazazi, walezi na watoa dira kwenye maisha ya watu wanaowafundisha hivyo wanapaswa kuthaminiwa.
"Nipende kuwashukuru hawa walimu, wamefanya kazi kubwa na kutoa dira ya mwelekeo wa maisha yangu katika kipindi chote nikiwa kwenye chuo cha ualimu cha Katoke", alisema Dk Biteko.
Walimu waliopokea tuzo hizo ni pamoja na Mwalimu Justin Temihangwa ambaye kwa sasa ni mstaafu pamoja na Martin Mwombeki ambaye pia ni mstaafu.
Hafla ya siku ya walimu duniani huadhimishwa kila tarehe 5 mwezi wa Kumi kuenzi na kuthamini mchango wa walimu duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko katika Sekta ya Elimu yanaanza na Mwalimu mwenyewe.
Sherehe hizo za Siku ya Mwalimu zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba na baadhi ya Wabunge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan alisema kuwa, Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za Walimu nchini hatua kwa hatua ikiwa ni pamoja na kuwapandisha Madaraja na kutoa malipo ya stahiki mbalimbali.
Rais, Samia alisema hayo alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nisahti kwenye maadhimisho ya Walimu duniani kiwilaya zaidi ya 2000 wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita wakati akitoa salamu za Siku ya Walimu Duniani kwa mwaka 2023 .
" Walimu ni jeshi kubwa na Serikali inathamini mchango mkubwa mnaoutoa, Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zenu ili hali zenu ziwe bora zaidi, hivyo nimemwagiza Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko awasikilize kisha aniletee maazimio mliyoyafikia ili niyafanyie kazi" alisema Rais Samia.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Shigela alisema Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu kwa miamka miwili Mkoa wa Geita imejenga nyumba za waili 63 licha ya kuwa na shule 963 kwa mwaka huu serikali imejenga maabara 116 na mabweni 74 yamekamirika.
MWISHO
Comments
Post a Comment