MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA BUKOMBE AMEWATAKA WANACHAMA KUANZISHA MIRADI KATIK KATA NA MATAWI ILI JUMUIYA ZIWEZE KUJIENDESHA
Ameyasema hayo alipofika Kwenye kata ya Namonge katika ziara ya kata kwa Kata kwa viongozi wa Jumuiya ya Viongozi wa Jumuiya tatu UWT,UVCCM NA WAZAZI Wilaya ya bukombe ilionza leo tarehe 24.10.2023
Pia amewataka wanachama kulipa ada ili waweze kuwa wanachama hai kwani kulipa ada kuna faida kwenye jumuia mpaka chama kwani chama kitaweza kujiendesha.
Halikadhalika Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Bukombe Julieth simon Nibaze amewataka Wenyeviti wa kata na Matawi kufanya vikao kwa kufuata kanuni na kalenda za vikao
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga Ndugu amewataka Wanachama wa CCM kuziunga mkono Jumuiya zote ili kufikia malego waliojiwekea.
Comments
Post a Comment