Ernest Magashi
Bukombe. Madiwani wa halmashauri ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na watalamu kwa kuwahudumia wananchi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kwenye baraza la madiwani baada ya uchaguzi wa makamu mwenyekiti na wenyeviti wa kamati za kudunu.
Nafasi hiyo ya umakamu Mwenyekiti ikichukuliwa na diwani wa kata ya Lyambamgongo Boniohance Shitobero baadavya kuoigwa kula za ndio madiwani wote walisema ndiyo makamu mwenyekiti wa zamani diwani viti malumu Leokadia Kasase alikubari matokeo na kupisha kiti hicho kwa kuzingatia kanuni.
"Nawaomba uongozi mpya wa halmashauri kujenga upendo na wenyeviti wa kamati za kudumu za halmashauri sisi hatutaraji kuwa na baraza la madiwani lenye migogoro na watalamu natamani kuona munachapankazi kwa upendo na mshuoamano mkubwa kwa kuzingatia mipaka na kushugulikia matatizo ya wananchi kwa wakati", alisema Nkumba.
Makamu mwenyekiti aliyemaliza muda wake Leokadia Kasase akitoabshukrani kwa madiwani walivyo mpa ushirikiano wakati wa uongozi wake aliwaomba madiwani na mkurugenzi mtendaji na watalamu wengine kuendelea kumpanushirikiano kwa nafasiyake ya udiwani.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Shitobero aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura za ndiyo licha ya kumpa nafasi hiyo aliwahidi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na kibari kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri Yusuph Mohamed.
"mimi kiumri nimkubwa ila kimadaraka mimi nimdigo niitakueshimu mwenyekiti ninaomba madiwani na watalamu kunipanushirikiano na sitafanyia kazi maneno ya majungu", alisema Shitobero.
Mohamed akimkaribisha makamu mwenyekiti kwenyekiti chake aliahidi kutia ushirikiano kwa makamu usiku na mchana ili kuijenga Bukombe huku nafasi za wenyeviti wa kamati za kudumu zikichukuliwa na madiwani wengine baada ya waliokuwepo kutoridishwa na wajumbe.
MWISHO
Comments
Post a Comment