Runzewe Academy yatinga tatu bora Ligi ya Doto Cup 2023





Timu ya Runzewe Academy imeichapa goli 1-0 Timu ya Ushirombo Worriors na kutinga tatu bora katika mashindano ya Ligi ya Doto Cup 2023.


Mfungaji wa Runzewe Academy  Emmanuel Singi dakika ya 67 katika michuano ya kutafuta mshindi wa tatu kwenye uwanja wa Kilimahewa.


Katibu wa mashindano Domisian Kabalega amesema kesho kunamchezo wa fainali ya kusaka bigwa wa Doto Cup kati ya Butinzya Fc na Vetelane Fc Kata ya Bugelenga.


“Kabla ya fainali itatanguliwa na michenzo mbalimbali ikiwemo kukimbia kwenye magunia, kucheza bao, kukimbiza kuku, kuvuta kamba ma michezo mingine itakuwepo”Kabalega  amesema


MWISHO

Comments