NAIBU WAZIRI MKUU AAGIZA VYOMBO VYA DOLA KUSHUGULIKA NA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 


Enest Magashi,

Bukombe

Mbunge wa jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko ameviagiza vyombo vya dola kuzibiti na kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Dk Biteko akitoa shukurani kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara kata ya Bulenga wilayani Bukombe walivyo mwamini na kumchaguwa kuwa mwakirishi wao uchavuzi mkuu 2015 na Rais alimuona na kumuamini.


Akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Bulenga alilani vitendo vya kikatili vinavyo fanywa na baazi ya wanaume majumbani kwa kubaka watoto wao.


 "shuleni kunamatishio ya ubakani majumbani kunamatisho ya ubakaji haliambayo inatishia amani kwa watoto naagiza vyombo vya dola kushughulika na yeyote atakae bainika kufanya ukatili kwa watoto", amesema Dk Biteko.


Aliwaomba viongozi kulibeba na kukemea vitendo vya ukatili kila wanapo kuwa na mikutano ya hadhara na wakati wa kuhamasisha miradi ya maendeleo kwa kutoa elimu kwa wananchi kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Akizungumzia chagamoto ambazo zilielezwa na diwani wa kata ya Bulenga amesema wananchi hakikisheni maendeleo tunayatafuta wenyewe na Serikali itatukuta tunaendelea nataka niwaomba tumejenga shule za msingi na sekondari lakini mda sio mlefu madarasa ya taja nakwamba tuendelee kujenga miradi ya maendeleo", amesema Dk Biteko.


"Rais Samia Wanabukombe ametupa Eshima alinipa kazi ya kumsaidi Wizara ya Madini na ameniamni tena amenipa Wizara ya Nishati Naibu Waziri Mkuu nikwasababu ya wananchi nyinyi lakini Rais Saima sita muagusha hata nyinyi sita waagua nitawatumikia na Rais anatamani kila anapoenda akute wananchi wanahudumiwa nakelwa na watendaji wanao hujumu maendelo hivyo tumuunge mkono kwa kumuombea", aliongeza Dk Biteko.


Mwenyekiti wa halmashauri Yusupho Mohamed alisema kwa mwaka 2022/23 halimashauli ilipokea sh12.5bilioni zimeletwa Bukombe kwaa ajili ya miradi ya maendeleo.


Diwani wa kata ya Bulenga Erick Kagoma Serikali imeleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi aliahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Mbunge


Awali Mwenyekiti wa UWT , Taifa Mery Chatanda akiwa Wilaya ya Bukombe kwenye mkutano huo akiwaomba wanawake kuacha kufumia macho wanaume wanao baka watoto wakike wawashitaki kwenye vyombo vya dola ili kushugukikiwa na kukomeshwa vitendo hivyo


Wanawake wametakiwa kuwafichua wanaume wanao fanya ukatili kwa watoto wao wa kuwazaa harafu kinamama wanawafichia sili.


"kinamama amukeni kifikira kuacha kuwakumbatia na kuwafichia sili waume zetu wanao baka watoto harafu kesi inaishia kwa mwenyekiti wa kitongoji wapelekeni kwenye vyombo vya dola", alisema Chatanda.


Amesema Serikali inajenga shule lakini kunabaazi ya walimu sio wadilifu wanabaka wanafunzi na majumbani wanaume wapo nimeona niyaseme haya kwa sababu yapo kinamama yafichueni ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii ili tutegeneze taifa lenye madili.


MWISHO

Comments