MKURUGENZI MTENDAJI AAHIDI NEEMA KWA TIMU INAYOWAKIRISHA BUKOMBE DARAJA LA TATU











Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Lutengano Mwalwiba ameahidi neema kwa timu ya Bukombe Combine Sports Club itakapo fanya vizuri katika mashidano ya ligi ya daraja la tatu mkoa wa Geita.


Mwalwiba ameyasema hayo kwenye hafla fupi ya kuzindua logo ya timu hiyo na kutambulisha wachezaji ambao wamesajiliwa kwa msimu huu.


”Viongozi wa timu hii wameonyesha dira na jambo la kipeke katika Wilaya ya Bukombe na kwa kuonyesha ushirikiano kwa timu hii ambayo inawakilisha Wilaya yetu sisi kama halmashauri tunaahidi kuishika mkono ili iweze kufanya vizuri zaidi”Lutengano amesema


 Awali Katibu Mkuu wa Club hiyo ya michezo Ernest Magashi wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Club amesema iliazishwa Machi 6, 2021 na kusajiliwa baraza la michezo Tanzania  (BMT) Desemba 6, 2021.


Amesema kwa msimu wa mwaka 2022 wameshiriki michuano ya daraja la tau na FA katika mazingira magumu hali ambayo imewalazimu kushirikisha wadau mapema kwa ajili ya kihitaji  kushikwa mkono.


Nae Katibu wa Chama Cha Mpira wa miguu mkoa wa Geita Bosco Mwidadi amesema ili kuunga juhudi za mweshimiwa Mbunge wa jimbo la Bukombe ambayo amekuwa akifanya kila mwaka kwa kuaada ligi kuazia ngazi ya kijiji hadi Wilaya kunaumuhimu wa kuwepo timu  nzuri yenye viongozi wenye maono kama Bukombe Combine sports Club.

Comments