Madiwani wamewaomba wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Kata kuyasemea maendeleo yanayo tekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi wajue kazi kubwa vinavyo fanywa za kimaendeleo na Rais kwa kushirikiana na Mbunge Dkt. Doto Biteko.


Wito huo umetolewa na diwani viti Maalumu Pili Kondela kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Iyogelo ambayo imeletewa fedha nyingi toka Serikali kuu na mfuko wa Jimbo


Awali Diwani wa Kata ya Iyogelo Juma Lushiku amesema kwa mwaka wa fedha Julai 2021 hadi Juni 2023 shule ya msingi Shibigo imepokea Tsh milioni 31.2 toka serikali kuu huku Mbunge kupita mfuko wa Jimbo alitoa Tsh milioni 9.8 kwa ajili ya kukamirisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa.


Akiwapongeza wananchi Lushiku amesema katika mradi huo guvu za wananchi ni Tsh milioni 2.4 ambapo ilipelekea kuufanya mradi huo kuwa na thamani ya Tsh milioni 43.6.


Lushiku katika hatua nyingine amesema Serikali ilileta Tsh milioni 3.8 toka mfuko wa jimbo zikiwemo mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Iyogelo  pia walipokea sh 653000 za ukarabati ambapo nguvu za wananchi sh 3.5 milioni.


Diwani wa kata ya Ushirombo ambaye alikuwa mgeni mualikwa kwenye mkutano huo alimpongeza diwani wa kata ya Iyogelo na kuwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono jitihada zinazo fanywa na Serikali kwa kuleta maendeleo kwa wananchi.


MWISHO

Comments