DED BUKOMBE AFUNGUA MASHINDANO YA MWL DOTO CUP.









Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano G. Mwalwiba amefungua mashindano ya Mwl Doto Cup katika kata ya Bukombe tarehe 20 septemba, 2023 huku akiwataka waamuzi wa mashindano hayo kutenda haki wakati wote wa michezo.


"Waamuzi hakikisheni mnatenda haki ili kuleta usawa wakati wote wa michezo."


Aidha  amezitaka timu zote 17 za mpira wa miguu na 16 za netball kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo kwani michezo ni afya, michezo ni ajira na michezo ni urafiki.


Kwa upande Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni,  Sanaa na Michezo Jenipher Kisusi amemshukuru Naibu Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Biteko kwa kuanzisha mashindano ya Mwl. Doto Cup kwani mashindano hayo yamekuwa yakijenga mahusiano pia yamepelekea kutengeneza timu ya watumishi yenye wachezaji bora katika mchezo wa netball na mpira wa miguu.


Mashindano ya Mwl Doto Cup katika halmashauri ya Wilaya ya Bukombe yanahusisha Walimu na watumishi wasiowalimu  katika kata 17 za halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.


Comments