MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KIJIJI CHA INYARA GEITA.









Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Abdallah Shaib Kaim pamoja na wajumbe wake na viongozi mbalimbali wa wilaya ya  Geita Mkoani Geita wametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Inyara kata ya nyamigota na kuweka jiwe la Msingi katika mradi huo utakao wanufaisha zaidi ya wakazi 6,000 wa kijiji hicho.


Akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023 Meneja wa RUWASA Wilaya ya Geita Mhandisi  Sande Batakanwa amesema  ujenzi wa mradi huo  ulianza kutekelezwa Disemba 2021 na kukamilika juni 2023 ambapo kwa sasa upo kwenye hatua za uangalizi.


Mhandis Sande amesema mradi huo umegharimu milioni 463.97 na umekamilika  ambapo  umehusisha ulazaji wa bomba kilomita 13.28, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 225,000, vituo vya kuchotea maji 11 na kuwaunganishia wateja majumbani 36 pamoja na pampu ya kusukuma maji Lita 15,970 kwa saa ambapo wananchi zaidi 6000 wananufaika na huduma ya maji safi na salama.


Akiweka jiwe la msingi katika mradi huo Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Abdallah Shaib Kaim amesema baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wamefanya ukaguzi na kijilidhisha kikamilifu kuwa mradi huo uko vizuri ambapo kwa sasa wananchi wanapata huduma ya maji  huku akimpongeza mkazi wa kijiji hicho alietoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji cha mradi huo.


Ameipongeza RUWASA Mkoa wa Geita katika mwendelezo wa kutekeleza miradi ya maji katika mkoa huo kwa lengo ka kufikia adhia ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani  huku Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita Mhandis Jabiri Kayilla amesema kutokana na uhalibifu wa vyanzo vya maji unaofanywa na wananchi kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi umekuwa ukiathili  pakubwa upatikanaji wa maji  hivyo RUWASA  inajukumu la kuhakikisha inawapatia huduma ya maji safi na salama.

Comments