Miradi 11 yenye Thamani ya Tsh bilioni 1.4 Wilayani Bukombe Mkoani Geita, inapitiwa na Mwenge wa Uhuru minne kuzinduliwa na miwili kuwekewa jiwe la msingi mitano kuona na kutembelea mingine kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Hayo ameeleza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba wakati wa kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed kwenye uwanja vya serikali ya kijiji cha Bukombe leo Agost 6, 2023.
“Nakili kupokea Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilaya ya Bukombe utakimbizwa kilomita 124 na kufikia miradi 11 yenye thamani ya sh 1.4 bilioni nawakaribisha sana wakimbiza mwenge kitaifa na viongozi wengine “ amesema Nkumba.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed amesema Mwenge wa Uhuru ikiwa Wilaya ya Mbogwe umekimbizwa kilomita 145 na kukagua miradi ya maendeleo minane yenye thamani ya Tsh bilioni 1.8 hakuna mradi ulio kataliwa na mwenge.
“Nakili kukukabidhi mwenge wa Uhuru na wakimbiza mwenge sita wa kitaifa na wengine wakiwa salama na mshukuru Mungu mwenge wa Uhuru Wilayani Mbogwe tumeukimbiza salama na leo naukabidhi ukiwa salama na watakieni majukumu mema ya kukimbiza mwenge watu wa Bukombe mkiongozwa na Mkuu wa Wilaya kaka yangu Said Nkumba”, amesema Sakina.
Diwani wa Kata ya Bukombe Mhe Lozaria Masokola amesema kwa niaba ya wananchi kuwa wamefurahi sana serikali kupanga mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yafanyike kwenye Kata ya Bukombe ikiwa ni mara ya pili akiwa Diwani
MWISHO
Comments
Post a Comment