Watu sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhika baada ya gari waliyokuwa wamepanda kupata ajali ya kugongana uso kwa uso Kati ya Hiace na Roli Kata ya Uyovu Wilayani Bukombe.
Kamada wa Polisi Mkoa wa Geita Sofia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa dereva wa Haice alisinzia na alikuwa na mwendo kasi.
Kamada Jongo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:7 asubuhi katika mtaa wa Mzibira Kata ya Uyovu Tarafa ya Siloka Wilayani Bukombe ikiwa Haice ikitokea Kahama kuelekea Nyakanazi imegongana uso kwa uso na Roli lililokuwa linatokea Nyakanazi kuelekea Kahama.
“Ni kweli tukio hilo lipo na hapa natoka eneo la tukio kushuhudia ajali hiyo katika ajali hiyo wamekufa watu sita kati yao ni Dereva na Kondakta na abiria wanne wamefariki dunia papo hapo huku majeruhi wawili wamekimbizwa Hospitali ya Uyovu na kwa sasa tunavyo ongea hivi wamepewa rufaa ya kwenda hospitali ya Mkoa wa Geita kutokana na Hali zao kutokuwa nzuri”, amesema Kamanda Jongo.
Jongo Akitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto amewaomba kuchukua tahadhari wakati wote wanapokuwa wanaedesha ili kuepusha ajali ambazo sio za lazma vikiwemo vifo.
Shuuda wa tukio hilo mkazi wa mtaa wa Mzibira John Kulinda ambae ni mwendesha bodaboda amesema ilikuwa majira ya saa12 :55 asubuhi nilikuta ajali hiyo nilianza kuona miili ya marehemu maiti mbili baadae nikaona na wengine nikiwa na abilia wangu roho iliniuma sana sikufanya chochote niliamua kuodoka.
Diwani wa Kata ya Uyovu Mhe Inyasa Kulusanga amesema serikali ichukue hatua ya kujenga tuta eneo hilo la kuzuia mwendo kasi na kuendelea na utoaji wa Elimu kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto ili wajue athali za ajali.
Comments
Post a Comment