Timu 222 zimeanza kutimua vumbi katika viwanja vya michezo kwenyekata 17 wilayani Bukombe mkoani Geita kuwania ubingwa wa ligi ya Doto Cip 2023.
Hayo yameelezwa na katibu wa ligi ya Doto Cup 2023 Domisian Kabalenga jana Julai 4,2023 kwenye michezo ya ufunguzi wa ligi hiyo kata ya Bugelenga .
amesema lengo la mashindano hayo ni kuibua na kukuza vipaji kwa vijana wa Wilaya ya Bukombe ambao wanadoto ya ya kufika mbali kupitia vipaji vyao.
Amesema kwa mwaka 2022zilishiriki timu 175 huku 2023 zimeongezeka hadi kufikia timu 222.
Diwani wa kata ya Bugelenga Donard Lubigisa akizungumza kwa niaba ya mbunge wa Jimbo la Bukombe Dk Doto Biteko amesema mbunge tangu achaguliwe 2015 amekuwa akifanya mashindano haya kila mwaka ikiwa ni kuwaunganisha wananchi wa jimbo lake na kuibua vipaji kwa vijana.
Timu hizo zinacheza kwa mtindo wa kupigwa na kwenda na wanashindania fedha, vifaa vya michezo na kombe la Doto Cup 2023.
Katika ufunguzi huo zilicheza timu ya mashabiki wa Simba na Yanga ambapo Mashabiki wa timu ya yanga wameibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu ya mashabiki wa Simba na goli la kwanza la mashabiki wa Yanga lilifungwa na
Bathromeo Richard dakika ya 20 na magoli mengine ma willi yalifungwa kwa mikwaju ya penati na mashabiki wa timu ya yanga.
MWISHO
Comments
Post a Comment