KILIMAHEWA FC YATOA KICHAPO CHA 7-0 KWA BODABODA FC

 

Timu ya Kilimahewa fc imeipa Kickapoo cha magori 7-0  dhidi ya timu ya Bodaboda fc katika uwanja wa Kilimahewa kata ya Katente ikiwa ni michuano inayo endelea kila kona  kutimua vumbi ligi ya Doto Cup 2023 Wilayani Bukombe Mkoani Geita.


Wafungaji wa magori ya Kilimahewa fc ni Jeremia Aran dakika ya 15 gori la pili limefungwa na  Mrisho Sabiti dakika ya 41 huku mchezaji  Bagara Thomas akifunga dakika ya 50.


Gori la nne likiweka wavuni na Mrisho Sabiti dakika ya 79 gori la tano likapachikwa na Mambo Wiliam dakika ya 81 na dakika ya 87 gori la saba lilifungwa na  Samson Samson dakika ya 89.


Nohodha wa timu ya Kilimahewa fc Mbagara Thomas amesema matokeo hayo wameyapata kutokana na Ushirikiano wao uwanjani na kwamba wanamalengo makubwa kwenye ligi ya Doto Cup 2023.


Nahodha wa timu ya Bodaboda fc Faida Sango amesema matokeo waliyo yapata ni kutokana na makosa ambayo wameyaonyesha wachezaji wezake wakati wa mchezo ila wametoka watajipanga mwaka kesho.


Katibu wa ligi ya Doto Cup wilaya ya Bukombe Domisiani Kabalenga amesema ligi mwaka huu imeshirikisha Timu 222.

Comments