Timu ya Cholongo Fc iliibuka na ubingwa wa ngazi ya Kata baada ya kupata gori 4-1 dhidi ya timu ya Msinila Fc katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Mratibu wa Mashindano Ligi ya Doto Cup 2023 Bosco Mwidadi amesema magori ya Cholongo Fc yalipatikana kwa njia ya mikwaju ya penaliti na kupata ubingwa kwa mbinde jambo ambalo ni Tofali na miaka mingine kwa Timu hiyo.
Amesema kupitia ushindi huo Cholongo Fc imefuzu kushiri Lig hiyo Ngazi ya Tarafa na kwamba zimebaki Timu chache kumaliza mzinguko wa kata zote 17 ambapo wiki hii Ligi ya Doto Cup itaaza kwa ngazi za Tarafa kwa kuwakutanisha mabingwa wa kata zote
Katika mchezo huo dakika 90 zilimalizika hadi kipenga cha mwisho mwamzi anapuliza ilikuwa 0-0 kwa timu zote
Comments
Post a Comment