HUDUMA YA MAJI YAWAFIKIA WAKAZI WA KIJIJI CHA KATOME BUKOMBE GEITA.


 

Changamoto ya Wakazi wa kijiji cha katome kata ya katome Wilaya ya Bukombe mkoani Geita ya kufata maji umbali mrefu imefika mwisho baada ya Wakala wa maji na usafi  wa mazingira vijijini RUWASA Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho. 


Wakizungumza mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela kuweka jiwe la msingi katika mradi huo Wanachi hao wamesema kabla ya mradi huo walikua wakitumia zaiidi ya masaa saba kufata maji umbali mrefu hali iliyokuwa ikisababisha migogoro katika ndoa zao pamoja na kutumia maji yasiyo safi na salama.


Akisoma taarifa ya ujezi wa mradi huo mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bukombe Mhandisi James Moise amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 85 ukihusisha ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita laki moja juu ya mnara wa mita 12, vituo 13 vya kuchotea maji, ujenzi wa nyumba ya pambu, mtandao wa bomba kilomita 13.5, ambapo kwa sasa wananchi wameanza kupata huduma ya maji.



Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi juni 2022 na unatarajiwa kukamilika juni 2023 ambapo ulipangiwa zaidi ya milioni 449.6 na pindi utakapo kamilika utasaidia kupunguza changamoto ya kufata maji umbali mrefu pamoja na  magojwa yanayosababisha na matumizi ya maji yasiyo safi na salama kwa afya zao.


Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita mhandisi Jabiri Kayilla amesema mradi huo ni mwendelezo wa kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa miradi ya maji ambapo kwa mwaka  wa fedha 2022/2023 RUWASA mkoa wa Geita ulitengewa zaidi ya bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji mkoani humo.


Aki


weka jiwe la msingi kwenye mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amelizishwa na ujenzi wa mradi huo na amewapongeza watendaji na viongozi wa RUWASA Mkoa wa Geita kwa kutekeleza vizuri adhima ya serikali ya kumtua ndoo mama kichwani kutokana na kasi ya miradi ya maji vijijini mkoani humo.



Shigela amewataka wakazi wa kijiji cha katome kuwa walinzi wa kwanza wa mradi huo kwa kuhakikisha wanatunza kwa ajili ya matumizi ya mda mrefu pamoja na kuwataka wananchi hao kutumia fura ya mradi huo kuvuta maji majumbani kwao ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji.

Comments