WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUZAMA MAJI GEITA


Wat


u  watatu wamefariki dunia na wengine watatu kunusurika katika kijiji cha Nungwe halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo kwa kuzama majini ndani ya ziwa Victoria  wakati wakivua samaki baada ya chombo chao cha uvuvi (Mtumbwi) kuingiza maji ndani nakusababisha kuzama.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi  wa Jeshi la zima Moto na uokoaji wilaya ya Geita Wambura Fidel amesema wavuvi hao walikuwa sita kwenye chombo cha uvuvi ambapo watatu wamefariki na wengine watatu waliokolewa na wavuvi walio kuwa kalibu baada ya mtumbwi waliokuwa wanatumia kuingiza maji nakusababisha kuzama ndani ya ziwa victoria.


Amesema kutokana na kasi ya maji yaliyokuwa yanaingia kwenye mtumbwi  baada ya chombo chao kutoboka yaliwashinda hivyo kupelekea kifo cha wavuvi hao amewataja waliofariki ni David Maliyatabu (25) mkazi wa nugwe, Kamuli Mhoja (20) mkazi wa nungwe na Faustine Cleophance (28) mkazi wa nungwe.



Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amefika katika eneo la tukio ambapo amewataka wamiliki wa vyombo vya uvuvi (Mitumbwi) kuhakikisha vyombo vyao haviingii majini bila maboya ya kuokolea pamoja na kufanya ukarabati wa mitumbwi hiyo ili kuepuka ajali za majini.


Naye miongoni mwa manusura wa ajali hiyo Dickson Alphonce  ameeleza  ajali ilivyotokea ambapo amesema  mtumbwi waliokuwa wanatumia ulianza  kuvuja  maji yakaanza kuingia ndani  baadae mtumbwi huo ulizama ndipo walipojirusha kwenye maji kila mmoja kwa lengo la kujiokoa.

Comments