RCCE KUANZA KUTOA MAFUNZO YA MAGONJWA YA MLIPUKO- BUKOMBE

.


Viongozi wa madhehebu na Waganga wa tiba asilia wilaya ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kuwa sehemu ya uelimishaji jamii juu  ya kujikinga na magonjwa ya milipuko.


Wito huo umetolewa na Ofisa program ya uelimishaji, uhamasishaji, ushirikishwaji wa jamii wizara ya Afya Magdalena Dinawi wakati wa kikao cha kuunda kamati ya uelimishaji na uhamasishaji na ushirikishwaji wa jamii kujikinga na magonjwa ya milipuko wilaya ya Bukombe yenye wajumbe 45.



Dinawi alisema waganga wa tiba asilia waache tabia ya kupokea wagonjwa na kuanza kuwatibu bila kujiridhisha ugonjwa gani licha ya kudai wanatibu kwa kutumia mizimu kugundua chanzo cha magonjwa hali ambayo inaweza kusababisha milipuko ya magonjwa.


Aliwaomba viongizi wa madhehebu ya dini  kuacha kutumia maombi kila magonjwa badalayake watu wapimwe kwanza na huduma za maombezi ziendele.


Makamu askofu jimbo la Katoliki Kahama Piter Kadundu alisema wao kama viongozi wa dini wamekuwa wakitoa Elimu ya kujikinga na magonjwa ya milipuko na kwamba jamii ilipata maelekezo ya wizara ya Afya tangu mlipuko wa Uviko -19.



Kadundu alisema kuundwa kwa kamati ya kuelimisha jamii kujikinga na magonjwa ya milipuko ifanye kazi kwa kutoa elimu kwenye jamii.


Mwenyekiti wa Umoja  wa Waganga na Tiba asili (UWAWABU) Wilaya ya Bukombe Mohamed Hames kwa jina marufu supu ya Mamba alisema elimu aliyoipata ataifikisha kwa wezake.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akifunga kikao cha kuunda kamati cha RCCE aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini na waganga wa tiba asilia pamoja na wajumbe wengine kutekeleza majukumu ya kuhamasisha jamii kujikinga na magonjwa ya milipuko kwa kukaa mazingira safi  n kujenga vyoo.


Nkumba aliwaomba waganga wa tiba asili kuruhusu wagonjwa kwenda hospitali kupima afya kabla ya kuanza kutoa huduma ili kujikinga na mikipuko ya magonjwa

"




Comments