Rais Samia: Sekta ya madini kuchangia 10% Pato la Taifa mwaka 2025.

 


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo April 17, 2023 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano kati ya Serikali na Kampuni tatu za madini kutoka Perth Nchini Australia ambapo amemuomba Waziri Mkuu Majaliwa kwenda kuwaambia Wakazi wa Lindi wachangamkie fursa za mradi wa madini Chilalo na LNG na kusema kwa sasa Lindi ni Matajiri na sio Wanyonge.




Akiongea baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Ikulu Chamwino Dodoma Rais Samia amesema “Hadi sasa kuna kiasi cha mashapo cha tani milioni 67 zenye wastani wa 5.4% ya madini ya Kinywe (Graphite), yaliyogunduliwa katika kijiji cha Chilalo (Lindi) ambayo ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 18”


“Miradi hii mitatu ni miradi mikubwa lazima ilete manufaa kwa Taifa, Watanzania tujipange kwenda kutoa huduma za chakula, mafuta n.k Watanzania tuwe tayari kwenda kutoa huduma, tukalishe chakula kwenye migodi hii”


“Hapa nataka niseme na Ndugu yangu Kassim Majaliwa (Waziri Mkuu) Lindi kuchele, tunaanza na miradi hii na LNG ipo njiani inakuja, kaseme nao Ndugu zetu kilugha kule wakuelewe wajipange kwenda kutoa huduma katika maeneo hayo Lindi sasa sio Mkoa mnyonge lakini ni Mkoa Tajiri, hongereni sana”


“Mikoa ya Lindi na Morogoro ipo katika ukanda wa madini Kinywe (Graphite) na Mkoa wa Songwe upo katika ukanda wenye madini adimu “rare earth element” ndio maana miradi hii ipo Chilalo (Lindi), Epanko Wilayani Ulanga na Ngwala wilayani Songwe”


“Hadi sasa kuna kiasi cha mashapo cha tani milioni 67 zenye wastani wa 5.4% ya madini ya Kinywe (Graphite), yaliyogunduliwa katika kijiji cha Chilalo (Lindi) ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 18, Tani milioni 63 zenye wastani wa 7.6 % ya madini ya Kinywe yamegundulika katika eneo la Kijiji cha Epanko ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 18

Comments