MWIZI WA KUKU ANUSURIKA KIFO KWA KIPIGO CHA WANANCHI BUKOMBE

 


Mkazi wa kijiji Kashero  kata ya Lulembela wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Alex Masweng'hwa amenusurika kifo kwa kupewa kipigo na wananchi wakimtuhumu ameiba kuku wa kienyeji wa wili wenye thamani ya sh 25000 ambapo hakutaja alipo waiba.


Alex alikamatwa na wanachi katika mtaa wa kapela mjini Ushirombo wilayani Bukombe akiwa anatafuta wateja majira ya saa 11: 00 alfajili ya kuamkia jana.


Mkazi wa Ushirombo Yohana Musa ambae alikutana na Alex.


"yakiwa majira ya aruyfaji nilikutana na kijana Alex anakuku wa wili nikamuuliza vipi hawa kuku unauza Alex akajibu anatafuta wateja ndipo nikamwambia twende nikaone unapo fugia kuku make sasa hivi kuna wimbi la wizi wa kuku sana kwenye majumba ya watu Alex akaniambia twende" na kuongeza kuwa.


"tulipo fika sitendi ya Mabasi makubwa mjini Ushirombo akasema "oya" nikwambie ukweli hawa kuku nimeiba naomba uniache tu nikauze na tafuta hela ya unga ndipo nilimwabia twende kwa wezangu tulifika hapo akawekwa chini ya ulinzi", alisema Yohana. 


Mkazi wa mtaa wa Kapela Doto Sulasula kutokana na wimbi la wizi wa vitu mbali mbaki majumbani hasa sikrini simu redio kubwa na kuku na bata aliomba Serikali kupambana na uharifu huo kwa kuzuia vijana kukaa bila kazi za kuwaigizia kipato halali badala yake wana vijiweni kucheza kamali na za kuneti  hali ambayo  huwashawishi na kupata tamaa ya kujiunga na vikundi vya uharifu.

 

Barozi  nyumba 10 mtaa wa Kapela Baridi Sambai amewaomba wakazi wa Eneo hilo kuweza kutoa taarifa za wagenibwanao wapoke kwenye familia zao wanao wapokea kutoka meaeneo mbalimbali ili viongozi wa serikali kuanzia shina ili kuzibiti wimbi la wizi.


Sambai aliwaomba vijana wabuni frusa za kiuchuki za kuwapatia pesa na kuachana na vikundi visivyo na faida ili kuepuka tamaa za kujiunga na vikundi vya kiharifu.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akidhibitisha tikio holo ofisini kwake amewataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu kwa kipigo badalay ake watoe taarifa kwenye vyombo vya dola hasa polisi.



"Wananchi niwaombe kuacha kijichukulia sheria mkononi mnapo kamata mharifu au kuhofia uharifu badalayake toeni taarifa kwenye vyombo vya dola, polisi ili wamchukue kisha afukishwe mahakamani" ameongeza kuwa kama wasigekuwa polisi kuwahi eneo la tukio baada ya kupata taatifa za watu wema kuwa kuna mwizi wa kuku anataka kuuwawa wasinge mkuta akiwa hai hivyo wananchi msijichukulie sheria mkononi", alisema Nkumba.


Nkumba alisema  hali ya kiusalama katika wilaya Bukombe iko salama na kwamba kuna watu wasiojulikana wameendelea kulipotiwa katika jamii wanajihusisha na uharifu na serikali kupitia vyombo vyake inaendelea kuwachuguza na hivi karibuni watakamatwa.


MWISHO

Comments