Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Hassan Mohamed ameiomba jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Hassan Mohamed ameiomba jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Mohamed ameyasema hayo wakati wa upandaji miti ya kivuli 200 katika shule ya Bungazu sekondari ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kilele cha wiki ya wazazi CCM ngazi ya Wilaya.
"Tumekuja kupanda miti kwa kutunza mazingira na nawaombeni sana walimu kuendelea kutunza uoto wa asili ili kuvutia mvua", amesema Mohamed.
Amesema licha ya Wilaya kuzungukwa na eneo kubwa la Hifadhi mbalimbali za uoto wa asili ni jambo jema kwa jamii kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa faida za kujikinga na ukame.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Bukombe Majaliwa Rajab amesema walianza utekelezaji wa upandaji miti sehemu mbali mbali katika tasisi za serikari za Afya na Elimu.
Alisema hadi leo Machi 31, 2023 wamepanda miti 1000 ikiwa lengo ni kutunza mazingira ambayo yanatakiwa yaendelee kutunzwa na jamii inayozunguka kwenye Taasisi hizo.
"Pamoja na kupanda miti hiyo 1000 kwenye Mataasisi pia tunaendelea kuihamasisha jamii kitunza mazingira" , amesema Rajabu.
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Uyovu Iddirisa Mgabe aliongeza kuwa ili kuendelea kutunza mazingira jamii inatakiwa kwenye kaya kutumza mazingira kwa kupanda miti.
Comments
Post a Comment