KESI YA KUVUNJA KANISA KUSIKILIZWA APRIL 12 GEITA


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita leo imeahirisha kusikiliza Shauri la Kesi inayomkabili Ndg.Elipidius Edward [22] Mkazi wa Kata ya Buhalahala wilayani Geita Mkoani Geita anayetuhumiwa kwa Makosa Mawili likiwemo kosa la kuvunja na kuingia kwenye Nyumba ya Ibada pamoja na Kosa la Kuharibu Mali za Kanisa.


Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo April 3 Mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Geita  Cleofas Waane ambaye Mnamo Machi 20 alijitoa kusikiliza kesi hiyo kutokana na Sababu ya kuwa yeye ni Mkatoriki ambapo shauri hilo alirejesha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Samwel Maweda.


Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Samwel Maweda ambaye pia Kesi hiyo aliipeleka kwa Bi.Johari Kijuwile Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Geita ambaye ndiye aliyepanga kusikiliza kutokana na sababu za kiafya shauri hilo limepangwa kusikilizwa April 12 , 2023 ndipo itakaposomwa na Kusikilizwa Kwa mara ya Kwanza katika Mahakama hiyo.


Ikumbukwe kuwa Kijana huyo Elipidius Edward anadaiwa kutuhumiwa kuvunja na kuingia kwenye Nyumba ya Ibada na Kuharibu Mali katika Kanisa kuu la Kiasikofu Jimbo Katoriki la Geita Mnamo Feburuari 26 Majira ya Saa nane Usiku Mkaoni Geita .

Comments