BUKOMBE COMBINE FC YAINYUKA GOLI 12 -3 MWALO FC

 



 Timu ya Bukombe Combine fc imeichapa goli 12-3 timu ya Mwalo wakati wamchezo wa kirafiki mchezo ukiofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwalo kata ya Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.


Wafungaji wa magoli ya Bukombe Combine fc Visent Buyenze dakika ya 18 na dakika ya 30 na dakika ya 46 huku mchezaji Wali Red akiwainua mashabiki wa Bukombe Combine fc dakika ya 68

Na Emmanuel Kabote dakika ya 22 na dakika ya 33 na dakika ya 75.


Wachezaji wengine waliofunga magori ya Bukombe Combine fc Shukuru Kalokeye dakika ya 79 Antony Mayoyo dakika ya 83 na 88.


Mfugaji wa magori ya Mwalo fc Zephania Peter dakika ya 44 na 69 na 77.


Nohodha wa timu ya Bukombe Combine fc Visent Buyenze akitoa shukurani kwa wachezaji wezake aliqnza kwa kumshukuru Mungu nakuongeza kuwa wamepata matoke hayo mazuri kutoka na kujiamnini wachezaji na kufata maelekezo ya mwalimu.


Buyenze amesema kuwa timu ya Bukombe Combane fc inaendelea na michezo ya kirafiki na timu mbalimbali kwa lengo la kujianda na ligi ya Doto Cup 2023 na ligi daraja la tatu mkoa wa Geita.


Nohodha wa timu ya Mwalo fc Mashaka Sanane amesema wamepokea matoke hayo kwa moyo mmoja na wezao wametumia makosa yao kuwafunga hivyo watajianda kwa ajili ya kuwafata Bukombe Combine fc.


MWISHO

Comments