AUWAWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA KISHA KUKATWA VIGANJA GEITA.




Mwanamke  Mmoja aliefahamika kwa jina la Milembe Seleman Mwenye umri wa miaka 43  Mkazi wa mtaa wa Mseto amekutwa Ameuwawa kikatili mtaa wa Mwatulole Kata ya Buhalahala  halmashauri ya Geita Mjini Mkoani Geita na watu wasiojulikana.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa jeshi la  Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi  Berthaneema Mlay Amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saamoja asubuhi.


Mlay amesema baada ya jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kufika katika eneo hilo wamekuta mwili wa marehemu umekatwa sehemu mbalimbali ikiwemo kichwani, usoni pamoja na mikono yote miwili huku mkono wa kulia ukiondolewa kiganja. 


Kamanda Mlay amesema watu nne wanashikiliwa kwa tukio hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku mwili huo mpaka sasa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.


Nao baadhi ya mashuhuda watukio hilo wamesema wameamka asubuhi nakukuta mwili huo wa marehemu akiwa umetelekezwa katika jengo ambao linadaiwa lilikuwa linamilikiwa na marehemu huyo.

Comments