AMUUA MWANAE KWA KUMBANA PUMZI KISA ULEMAVU GEITA


 



Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mtu mmoja alietambulika kwa jina la Elias Bakumye (32) mkazi wa kijiji cha Chikobe kata ya Butundwe wilaya ya Geita mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mwanaye mlemavu wa viungo na kumuzika porini.


Akithibitishakutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amesema mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka mitano na mwili wake uliokotwa na wasamalia wema Aprili 12 majira ya saa tatu asubuhi. 


Jongo amesema baada ya kupokea taarifa hizo walituma timu ya upelelezi kwenda eneo la tukio ambapo baada ya kufika eneo la tukio walikuta mwili ambapo ulionekana marehemu alikuwa ni mlemavu.


 “Alikaa na mototo akaona hawezi kuendelea kumuhudumia yule mtoto akaamua kumubeba yule mtoto kumpeleka kwa mama yake ambaye Alivyofika kule wazazi pamoja na yule mwanamke mtalaka wake wakakataa kumupokea yule mtoto alipofika eneo la porini hapo anakiri kwamba akaona yeye hataweza kumuuguza huyu mtoto kwa hiyo akamubana pumzi na kumuua na hatimaye akamufukia. Amesema Kamanda Jongo.


Kamanda Jongo amesema mwili ule ulikutwa umeshambuliwa na wanyama na kuonekana kupata michubuko kwenye maeneo tofauti ya ngozi ya mwilini.


Mpaka sasa mtuhumiwa amekamatwa na jeshi hilo la polisi na taratibu za kisheria zinaendelea na amewataka wakazi wa Geita kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya ukatili kwenye familia na maeneo wanayoishi.

Comments