WENJE, HECHE WASHINDWA KUHUTUBIA BUKOMBE


 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya Serengeti John Heche na mwenyekiti wa chama hicho na kanda ya Viktoria Ezekiel Wenje wameshindwa kuhutubia wananchi na wanachama wao kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umeandaliwa na viongizi wa chama hicho wilaya baada ya mvua kali kuanza kunyesha katika viwanja hivyo baada ya kukanyaga uwanja wa mkutano.

Wananchi na wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wametupia rawama viongozi wa chama hicho wa kada kwa kushindwa kutoa hotuba ya bila mziki hata kwa dakika 10 katika mkutano wa hadhara uliokuwa umeandaliwa huku wanachama wengine wametoka  mbali kuja kusikiliza viongozi wao.

kwa nyakati tofauti katika uwanja wa mkutano wa hadhara soko la zamani mjini Ushirombo kata ya Igulwa  mwanachama kutoka kijiji cha Bugando kata ya Iyogelo Sadick Sahani aliomba waongee japo  bila vyombo na wanachama wachache ila viongozi hao walikata.

Sahani alisema viongozi hao walitakiwa kuongea hata machache kwa kutambua uthamani wa wanachama kutokana na wanachama kuwasubiria kwa hamu tangu saa mbili asubuhi.

Nae mwanachama wa CHADEMA kata ya Bulangwa Lucey Amos alisema amejisikia vibaya viongozi hao kushindwa kutoa hotuba kwasababu wamewasubiria kwa hamu watoe ujumbe wa ziara ili wakawape wanachama wenzao.

Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya ziwa Zachalia Obadia aliwaomba radhi wanachama na wananchi wa wilaya ya Bukombe akiongeza kuwa wanataarifa kuwa Uyovu hakuna Mvua, Nyakanazi hakuna mvua na Biharamulo kunajua hivyo inawabidi waondoke wawahi huko badala ya kukaa kusubiri mvua ikate.

"niwaombe wanachi na wanachama kutambua kuwa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinakazi ya kuikomboa Bukombe na maeneo mengine na taifa kwa ujumla hivyo tunaomba mturuhusu tuondoke tukaendele na mapambano ya ukombozi", amesema Obadia.

Kufatia hali hiyo msafara ulielekea Runzewe huku wanachama na wananchi wakiwaacha wakiwa kwenye hudhuni huku wengime wakiraumu kupoteza muda kusubiri harafu viongozi hao wanafika na kuwanyoshea mikono na vidole na kuodoka.

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilaya ya Bukombe Joseph Mugana aliwaomba wanachama kukubaliana na matokeo ya mvua na kwamba amejitahidi kuwaomba viongozi hao hata abaki mmoja lakini wameomba waende.

Alisema wageni kitaifa katika mkutano huo alifika mwenyeki kanda ya vikitoria Ezekiel na mwenyekiti wa kanda ya Seregeti John Heche wote wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA taifa majira ya saa 6:47 mchana kabla ya dakika chache mvua kuanza kunyesha.



Comments