Waziri Mkuu atoa agizo hili kuhusu ukarabati ‘Mkapa Stadium’

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza haraka ukarabati wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa ili ukidhi mahitaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF baada ya kuufanyia ukaguzi hivi karibuni.

Ametoa agizo hilo leo Jumatano, Machi 1, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea kukagua hali ya uwanja huo baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo

“Ili mradi CAF wametupa onyo, ni onyo ambalo wametupa na muda wa kufanya marekebisho na muda huo waliotupa ni lazima tuanze jambo ndipo waridhie mambo mengine yaendelee, nimekuja kuwaambia msiruhusu uwanja huu umefungwa na CAF na kuzipeleka Timu zetu zikacheze ugenini”

Amesema kuwa kwakuwa CAF wameleta orodha ya makampuni yenye uwezo wa kufanya ukarabati wa kiwango cha juu hivyo Wizara itangaze zabuni ikiwezekana hata kwa mfumo wa ‘Single Source’ ili kazi ya awali ianze kufanyika katika maeneo ya kubadilishia nguo, vyoo, milango na bechi la ufundi

“CAF wakija hapa wakitukuta tunaendelea na kazi, wanaweza kuruhusu michezo mingine ichezwe ikiwa Timu zetu zitafuzu katika hatua za mbele tofauti na ambayo wameiruhusu sasa, tunahitaji haya marekebisho yafanyike kuanzia sasa, huu ni uwanja wa Taifa na zipo nchi za jirani ambazo zimeamua kuutumia uwanja huu”

.
.
.

.
.

Comments