MADIWANI KUSHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA


 Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wameadhimia kutunza mazingira ya kwenye vyanzo vya maji kwa kushirikisha wananchi.

Madhimio hayo yamefikiwa na madiwani leo Machi1, 2023 kwenye baraza la madiwani baada ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbogwe Mhandis Rodrick  Mbepera kuwapongezwa na madiwani kwa usimamizi wa miradi ya maji kwa kusamvaza huduma hiyo na wananchi asilimia 89 vijijini wanatumia maji safi na salama.

 Awali mhadis Mbepera aliliambia baraza la madiwani kuwa miradi mingi imwkamirika na kwamba kuna mradi wa maji kata ya Ng'homolwa ambao bado unachangamoto ya njia ya mabomba ya maji kutoka sehemu ambayo sio sahihi ila changamoto hiyo wanaishughukulia na itaisha.

"Miradi mingi ya imekamirika na inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi baada ya serikali kuleta fedha za miradi hiyo na kwamba ili miradi iweze kuto huduma kwa wananchi madiwani nawaomba sana kwa kushirikiana na wananchi kutinza mazingira ya kwenye vyanzo vya maji," amesema Mhandis Mbepera.

Diwani kata ya Masumbwe Harid Komolola amesema kwa idara zote ambazo zilihamishiwa serikali kuu kutoka halmashauri Ruwasa wamefanya kazi nzuri kwa kutandaza maji safi na salama vijijini haliambayo ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi kunya maji ambayo sio safi na salama na kusababisha magonjwa ambayo yanatokana na kinywa maji siosafi na salama.

"Licha ya pongezi hizo madiwani mtakubariana na mimi idara zote ambazo zikihamishiwa serikali kuu kutoka halmashauri maofisa wa Ruwasa wanachapa kazi wanasitahili pongezi ingawa na TARURA wanapambana hivyo ili kulinda vyanzo hivi vya maji tushikamane na wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kando ya vyanzo vya maji.

Hoja hiyo ya utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji  ikiungwa mkono na diwani wa kata ya Nyasato John Nzela na kuongeza kuwa kwa kazi ambayo imefanywa na maofisa wa Ruwasa halmashauri ione utaratibu wa kutoa hata cheti cha pongezi ambacho kitaandaliwa kupitia mapato ya ndani.

"Kwa kazi ambayo imefanya na Ruwasa kwa kuboresha maadhimio ya madiwani kutunza mazingira ya vyanzo vya maji safi na salama tuone umuhimu wa idara hiyo kwa kazi ambayo imefanya nzuri ipewe hati ya pongezi nasio kupigiwa makofi tu ingawa niadimu kwenye idara zingine," amesema Nzela.

Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga amewaomba madiwani kuendelea kushirikiana na watalamu katika miradi ya maendeleo licha ya Ruwasa kuonekana kufanya vizuri haitakiwi wabweteke badalayake wahakikishe wanaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa kupanua mtandao wa maji vijiji kwa kuzingatia bajeti ya mwaka wa fedha.

"Nawaombeni sana madiwani wenzagu tuendele kushirikiana na watalamu wa halmashauri yetu ili miradi inayo letewa fedha na serikali iweze kukamirika kwa wakati na Ruwasa wasibweteke kwa pongezibhizo licha ya madiwani kuadhimia kutunza mazingira panueni mtandao wa maji safi na salama kwa kuzingatia bajeti zenu ili wananchi wafurahie serikali yao", amesema Maganga.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri Sinzya Nsika aliwaomba waofisa wa Ruwasa kuagalia kwa jicho la tatu mradi wa majo safi na salam kata ya Ng'homolwa ikiwa mradi huo serikali ilileta sh 1 bilioni na tayali sh 700 milioni amelipwa mkandarasi huku mradi huo ukiwa nachangamoto za maji kutoka nje na mifumo ya bomba.

"Nawaombeni watalamu hasa watalamu toka ofisi ya Ruwasa kuboresha miundombinu za maji kwenye kata hiyo kwa fedha mabazo mkandarasi hajalopwa ili mradi huo usionekana uko chini ya kiwango", amesema Nsika.

MWISHO.

Comments