MAAFISA 17 WAKABIDHIWA PIKI PIKI ILI KUWAFIKIA WANANCHI KWA WAKATI


 Maofisa watendaji wa kata wilaya ya Mbogwe mkoani Geita  wamekabidhiwa pikipiki ambazo zitarahisisha utendaji kazi wao nakuwarahisishia kukusanya mapato ya ndani.

Hayo yameelezwa  na Mbunge vitimalumu mkoa wa Geita Rose Businga kwenye hafla ya kukabidhiwa pikipiki sita kati ya 17 zinazo hitajika ambapo hafla hiyo imefanyika makaomakuu ya halmashauri ya Mbogwe kata ya Mbogwe.

Businga alisema serikali inatambua umuhimu wa watumishi wa kada zote hivyo imeaza na watendaji wa kata kuwapa pikipiki na usafiri huo ukawe chachu ya maendeleo kwa kila kata kwa kuhudumia wananchi na kukusanya mapato ya serikali.

Awali Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbogwe Egidius Kahendaguza alisema serikali imeleta pikipiki sita katika mgao wa kwanza wanatarajia kupokea pikipiki 11 zingine katoka mgao wa pili kutokana ombi la Mbunge Businga kuibuwa hoja Bungeni akiomba serikali itoe pikipiki kwa maofisa watendaji wa kata ili ziwarahisishie utendaji kazi.

 Ofisa mtendaji wa kata ya Ngemo Vinitha Edward alisema kabla ya kupata usafiri walikuwa wanapata changamoto kubwa kuwafikia wananchi kutatua kero lakini kwa sababu serikali imewapa usafiri utakao rahisisha utendaji wao watawafikia wananchi kwa wakati hata ukusanyaji wa mapato utapanda.

Mwenyekiti wa maofisa watendaji halmashauri ya Mbogwe Ntembanda Lug'wecha alisema pikipiki 11 zilizobaki zisichelewe badala yake ziwahi ili na watendaji wegine waliobaki waweze kutekeleza majukumu yao kwa kufika ambapo walikuwa hawawezi kufika kutokana na ukosefu wa usafiri.

Lug'wecha alisem piki piki hizi zitawapa msukumo wa utendaji kazi kuwafikia wananchi kwenda kutatua kero na changamoto kwa wakati hivyo serikali iendelee kuwaboreshea mazingira watumishi wa umma wa kada zote kuanzia ngazi ya chini.

Kaimu kamanda wa polisi wilaya ya Mbogwe mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Denis Rwehumbuza alitowa wito kwa maofisa watendaji wa kata kutunza vyombo hivyo vya moto amewaomba wanapo endesha kuzingati sheria za barabarani ili kuepuka ajari zisizo za lazima.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Visent Businga aliongeza kuwa kuwepo kwa piki piki hizo utaleta tija nabufanisi mkubwa kwa watenda wa kata wanapo tekeleza majukumu yao haliambayo itaifanya halmashau kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

MWISHO

Comments