KAMATI YA SIASA CCM YA KOSHWA NA MRADI WA UMEME IGULWA

 

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata hiyo na kukoshwa na utelezaji wa miradi ukiwemo wa umeme ulioahidiwa kwa wananchi na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt Doto Biteko.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM kata ya Igulwa Ndg Bernedict Yohana alipo kuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi mikubwa ya maendeleo iliyo letewa fedha na Serikali kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.


Kamati ya siasa ya kata ilitembelea miradi mbali mbali ikiwemo shule ya msingi shikizi Kelezia, Mradi wa Umeme unaotekelezwa kuanzia kitongoji na Kijiji cha kelezia ambapo mradi huoutafungiwa Transforma mbili moja ndogo itakuwa ya kusambaza umeme kwa wananchi na Transfoma nyingine kubwa itakuwa itafungwa kwa ajili ya Mgodini namba mbili.

Alisema mradi huu unatekelezwa fedha toka Serikali kuu Tsh milioni 75 kilio cha wananchi na wachombaji wa madini ya dhahabu kumweleza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dk Biteko wakati wa ziara yake ya kwenda anahamasisha maendeleo na kusikiliza kero kwa wananchi Julai 15, 2022 kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika kata ya Igulwa kitongoji cha Kelezia.


Kamati ya siasa ilitembelea miradi mingine  ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa shule ya sekondari Doto Biteko na ujenzi wa Zahanati kitongoji cha Msufini (Buntubili), walitembelea na Eneo lililonunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Msinila, na walitembelea mradi wa maji ya Bomba ulioko Kitongoji cha Butambala


Yohana alisema llani ya Chama Cha Mapinduzi CCM aliwaomba viongozi wa Serikali kusimamia na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ambayo haija kamilika ili wananchi wapate huduma karibu Kama inavyo elekeza ilani ya CCM.


Alisema CCM imejiwekea adhima ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa ujumla kwa kutekeleza miradi mbalimbali na miradi hii itasaidia kutatua kero za wananchi  kufatabhuduma umbari mrefu.


Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM kata ya Igulwa Jonathan Samwel alimpongeza  Mbunge Dkt Biteko kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake   kwa wananchi.



Samwel alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa kwa kuendelea kuwajali wananchi kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo.

Afisa mtendaji wa Igulwa Valeli Kamuntu Rwela alisema amepokea pongezi na ushauri wa chama nakuahidi kuwa ataendelea kusimamia miradi ili ianze kutoa huduma kwa wakati.

Comments