HALMASHAURI KUANZA KUGHARIMIA WALIMU WA MICHEZO



Halimashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita imeahidi kusomesha walimu wa michezo ili kukabiliana na upungufu wa walimu wamichezo mbali mbali wilayani hapa.


Ahadi hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi mtendahi wa halmashauri hiyo Piter Ntaramka wakati akifunga mafunzo ya walimu wa michezo ya siku tatu katika uwanja wa shule ya sekondari Ushirombo akidai  halmashauri ina uhaba wa walimu wa michezo.


Katibu wa mafunzo Jackison Kusekwa alisema mafunzo hayo ya Kid's Athletics wilaya ya Bukombe ya lihudhuliwa na  walimu wa michezo 109 kati yao walimu 75 kutoa shule za msingi huku 34 kutoa shule za sekondari.


Kusekwa alisema malengo ya mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu wote kupata ujuzi na uwezo wa kufundisha wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne pia mafunzo haya yatasaidia kupunguza utoro mashuleni  msingi na sekondari.



Kusekwa alisema kupitia mafunzo hayo wamefundishwa michezo mingi ikiwemo Formula one, Frog jump, Target throwing, Cross hopp, Overhead throwing.


"Kupitia mafunzo haya tumegundua kuwa Athletics  ni mchezo mama wa michezo yote ikiwemo mpira wa miguu, Volleyboll, Netboll, Basketboll na mitupo," alisema Kusekwa


Afisa michezo  toka baraza la michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu akielezea kuazishwa kwa michezo hiyo kimataifa lengo nikuwaada watoto mashuleni na wegine ili waweze kuchagua michezo wanayo ipenda.


Akishukuru kwaniamba ya washiriki wezia Mwalimu Ezekiel Mirambo alisema mafunzo waliyopatiwa yataleta matoke mazuri  mashuleni na hawataraji kwend kutunza vyeti walivyo pata lwenye mafunzo badalayakewata watajikita kufundisha ili kupata matokeo makubwa  kwenye mashindano yanayo lenga wanafunzi wa shule za misingi na sekondari.


Afusa michezo wilaya ya Bukombe Jenipha Kisusi liwaomba walimu waliopatiwa mafunzo kuwa chachu kwa walimu wezao katika kufundisha michezo shuleni kwa kuzingatia maelekezo ya mkufunzi toka BMT.


Comments