Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa nchi Zisizofungamana na Upande Wowote kuendelea kushirikiana katika kutumia fursa, kukuza biashara ya kimataifa na
uwekezaji, kushirikishana mbinu bora na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
Makamu wa Rais amesema hayo katika mji wa Baku nchini Azerbaijan, alipokuwa akihutubia
mkutano wa nchi Zisizofungamana na Upande Wowote, mkutano uliolenga
kujadili namna ya kukabiliana na athari za UVIKO – 19.
Amesema janga la UVIKO – 19 limetoa somo la kutotegemea
msaada wakati wote, hivyo inapaswa nchi wanachama kuwekeza katika tafiti na maendeleo kwa ajili ya kutatua changamoto za ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa chanjo, vifaa tiba, vitendanishi na
bidhaa nyinginezo za kuokoa maisha ya wananchi.
Dkt. Mpango pia ametoa wito kwa nchi Zisizofungana na Upande Wowote kuhakikisha
zinaimarisha uwezo katika ufuatiliaji, ili kutambua kwa wakati na kuzuia
magonjwa ya kuambukiza.
Akitoa uzoefu wa Tanzania katika kukabiliana na athari za UVIKO -19, Makamu wa
Rais amesema serikali ilihamasisha utoaji chanjo na kusambaza chanjo kwa walengwa, hatua ambayo ilisaidia katika kudhibiti janga hilo, kuongeza miundombinu
za kutolea huduma za afya pamoja na kuongeza watoa huduma, vifaa tiba na dawa muhimu.
Hatua nyingine ni pamoja na kutumia mkopo
wa masharti nafuu chini ya dirisha la Rapid Credit Facility (RCF) kutoka Shirika
la Fedha Duniani, ili kuongeza uwezo wa miundombinu katika elimu
Comments
Post a Comment