Cornel Magembe
Mkuu wa wilaya ya Geita
Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe ameonesha kusikitishwa na Matukio ya mauaji yanayojirudia marakwamara katika wilaya ya Geita hali inayopelekea kutishia usalama wa wakazi wa wilaya hiyo mpaka kupelekea kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo kuingilia kati tatizo hilo.
DC Magembe amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha kilichofanyika katika ukumbi wa EPZA mkoani Geita.
Amesema sababu mbalimbali zinazochangia kwa kiasi kikubwa mauaji hayo kuongezeka kila mara ni pamoja na wivu wa mapenzi, imani za kishirikina na mambo mengine yanayochangia mauaji hayo hali ambayo inasababisha kuibua hisia mbalimbali kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Magembe amesema kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na jeshi la polisi Mkoani humo wametoa mafunzo kwa askari zaidi ya 301 kwa ajiri ya kupambana na uhalifu huo.
“mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tumejipanga tumefanya vikao jana na juzi na hata leo nimechelewa kufika hapa kwa sababu nilikua kasamwa ambako sasa tumeamua kufanya mafunzo kwa maaskari wetu kupambana na hiki kinachoendelea ili kama kuna watu ambao wanazani sasa wanaweza kuendelea na matukio ya mauaji,kuna watu maarufu wakata mapanga kuna watu sijui wanafanya nini wanafanya vitu vya ajabu sasa kiama chao kimekuja na mimi nimetoka kule nimehamasisha zaidi ya maaskari 301 ambao tumewapa mafunzo kwa mda wa mwezi mzima kwa kazi hiyo tu” amesema DC Magembe.
Constantine Morandi
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi amesema hali iliyopo kwa sasa katika mji huo sio nzuri kwani inapelekea kuchafua taswira ya wilaya hiyo kutokana na matukio hayo kutokea kila mara.
Katika kikao hicho cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita ambapo mbali na hilo madiwani wameibua changamoto ya ubovu wa miundombinu katika zahani na vituo vya afya katika halmashauri hiyo hali inayopelekea wamama wajawazito kujifungulia gizani hasa nyakati za usiku.
Wamesema katika zahanati pamoja na Vituo vya afya mbilimbali hasa ambavyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme na zahanati hizo nz vituo vya afya vinatumia sora huku zikiwa zimechoka na kushindwa kutoa mwanga wa kutosha hasa nyakati za usiku na kulazimu wamama kujifungua kwa njia ya tochi.
“Na hapa nilikua najalibu kuangalia mkurugenzi si ni mwanamke hivi yeye anajisikiaje kusikia wakina mama wanajifungulia gizani naamini haitachukua hata wiki sasa mama mkurugenzi wewe ni mwanamke,wanawake wenzio huko wanateseka unajisikiaje mama’’ amesema Elias Ngole Diwani kata ya Nyanguku.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Zahara Michuzi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na huku akisema halmsahuri hiyo itapeleka mtaramu mapema iwezekanavyo katika sehemu zote zenye changamoto hiyo ili kutatua tatizo hilo.
Comments
Post a Comment