WAZIRI MABULA AWATAKA WAKURUGENZI KUPIMA,KULINDA NA KUSIMIA MAENEO YOTE YA UMMA

 



WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula amewaagiza Wakurugenzi 

wote wa Mamlaka za Serikali za mitaa kupima, kulinda na kusimamia 

maeneo yote ya umma na maeneo ya wazi ili kuondokana na 

mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.


Agizo hilo alilitoa leo jijini hapa kwenye mkutano mkuu wa Nane wa mwaka wa bodi ya usajili wa wataalamu wa Mipango miji ambapo alisema kumejitokeza utaratibu mbaya na usiovumilika, wa kuvamia maeneo ya wazi, maeneo ya umma pamoja na maeneo hatarishi na kuyabadilisha kuwa ya matumizi mengine, hasa makazi. 


Amesema Maeneo hatari kimazingira pamoja na maeneo ya wazi, yakiwemo maeneo maalum kwa matumizi ya baadaye (land bank), yanapaswa kupimwa, kumilikishwana kulindwa dhidi ya wavamizi.


Alisema ili tuwe na miji nadhifu na iliyopangwa vyema katika nchi yetu hakuna budi kuanza kusimamia upangaji wa miji midogo na vitovu 

vya vijiji. 


"Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022 inaonyesha kuwa miji 

inakuwa kwa asilimia 4.8 na taarifa tulizonazo tuna jumla ya miji midogo 

inayochipukia 4310 nchini ambayo isiposimamiwa ipasavyo itakuwa miji 

holela ya baadae," Alisema


Na kuongeza"Kwa kutambua umuhimu wa miji hiyo na uwepo wa kasi 

ndogo ya upangaji wa vijiji nchini, Wizara imeandaa mwongozo wa upangaji 

na ujenzi wa nyumba bora vijijini ili kuwezesha jamii yetu kuanza kupanga 

maeneo yao kuanzia vijijini," alisema waziri Mabula


Aidha alitoa maelekezo kwa Bodi ya Usajili wataalam wa Mipangomiji na wanataaluma wote kuweka mkazo Zaidi katika namna ya kuzuia miji yetu midogo na vijiji kuwa makazi holela yabaadae 

kwa kusimamia na kuelimisha jamii matumizi ya mwongozo wa upangaji na 

ujenzi wa nyumba bora vijijini.


Pia alisema Serikali itaendelea na jukumu lake la kuimarisha 

mahusiano ya kitaasisi ili kuimarisha maendeleo ya miji pamoja na kupata 

fedha kwa ajili ya kupanga na kusimamia miji.


Hata hivyo alielekeza kuwa gharama za kuweza kumudu kupanga, 

kupima na kumilikisha maeneo yote nchini ni kubwa,Ninaelekeza Mamlaka 

za Upangaji nchini kutenga fedha kutokana na mapato ya ndani ya kila 

mwaka, kwa ajili ya kazi ya kupanga,kupima, kumilikisha,kuendeleza 

na kusimamia miji katikamaeneo yao.


Akiongelea suala la Mabadiliko ya tabia ya nchi waziri Mabula alisema Ni suala muhimu sana kwa sasa katika sayansi ya usanifu wa miji duniani kote.


" Ili kukabiliana na 

mabadiliko ya tabia nchi katika miji yetu tunatarajia mchango mkubwa sana 

wa Wataalam wa Mipangomiji katika kuweka mifumo wezeshi kwa ajili ya 

kukabiliana na majanga mbalimbali kuanzia katika usanifu wa mipango 

kabambe ya Miji na mipangokina ya usimamizi wa uendelezaji wa Miji," alisema Waziri Mabula


Aliekeza katika suala la kuhimili janga la mafuriko mijini inahitajika, siyo tu 

kuimarisha uwekaji wa miundombinu kama mifereji ya maji yamvua, bali pia 

kuwekamiundombinu ya kijani kama vile maeneo chepechepe, maeneo ya 

Bafa (Buffer zones), mabwawa ya kuzuiamaji ya mvua (detention ponds) 

pamoja na maeneo ya kuwezesha maji kuzama ardhini (porous pavements)

ili kupunguza kasi na madhara ya mafuriko.


"Napenda nisisitize kuwa Maafisa Mipangomiji mmepewajukumu kubwa sana la kuongoza mwonekano wa miji yetu na vijiji kupitia taaluma mniyonayo. Ni matumaini yangu jukumu hilo mtalibeba kikamilifu na kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na kuzingatia kikamilifu matumizi ya takwimu mbalimbali za Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya majengo na takwimu nyingine kwa ajili ya kuwezesha utendaji kazi wenu kikamilifu," alisema


 Na kuongeza kuwa "Naelekeza  bodi ya Usajili Wataalam wa Mipangomiji kuongeza kasi na kuboresha mifumo 

itakayowezesha upimaji wa utendaji kazi wa kampuni na wataalam katika 

kutekeleza majukumu yao ya kila siku," alisema waziri Mabula


Watumishi na kampuni zitakazofanya 

vizuri katika upangaji mwone namna ya kuwapatia motisha na kujenga 

ushindani mzuri katika upangaji na usimamizi wa miji ili kuwa na miji salama, Jumuishi, stahimilivu na endelevu.



Pia Alisema Kwamba moja ya mahitaji makubwa katika upangaji wa miji endelevuna himilivu ni pamoja na upatikanajiwa takwimu sahihi zinazoendena na wakati. Ni wazi kwamba umuhimu wa 

takwimu hizi unajitokeza wakati wa kutoa maamuzi katika kipindi cha 

upangaji wa miji. 


Ni muhimu kujua idadi ya watu katika eneo la upangaji ili 

kujua ni mahitaji gani ya kijamii yanahitajika katika eneo hilo, kwa mfano 

idadi ya shule za msingi, shule za awali, zahanati, vituo vya Afya, maeneo 

ya kuchezea watoto Kwa kuwa sensa ya watu na makazi imefanyika 

August, 2022 ni vyema sasa takwimu hizo zitumike katika upangaji mipango 

ya uendelezaji miji.


Aidha, takwimu za umri, jinsi, idadi ya nyumba, idadi ya 

wakazikatika nyumba nk, zinatumiwa na wataalam wetu wa Mipangomiji 

katika kupanga mahitaji muhimu ya kijamii miongoni mwa rika mbalimbali, 

ikiwemo makazi ya wazee, mahitaji ya shule za awali, shule zaMsingi, 

Sekondari, mahitaji ya wenye ulemavu Takwimu na taarifa hizo zote 

zinapatikana kutoka katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.



"Miji ni eneo mojawapo katika kuleta maendeleo ya nchi

kupitia uwekezaji wa aina mbalimbali, ingawaje inaendelea kukumbwa na 

changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha miji yetu kutokutoa 

mchango uliotegemewa katika kuimarisha uchumi, kuongeza uhimilivu, na kuwa endelevu," alisema 



Na kuongeza "Mijiyetu inaukuaji wa mtawanyiko ambao unaongeza gharama za kuweka miundombinu kama ya maji,umeme, barabara nk, pamoja na gharama zakufuata mahitaji muhimu. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 tuna jumla ya majengo 14,348.372kati ya hayo asilimia 0.5pekee ndio majengo ya ghorofa," alisema. 



Alitoa rai kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Miji, Manispaa na Majijikupanga miji na kuifanya kuwa ya kiushindani kibiashara,kitalii, na kimazingiraili iweze 

kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, na kuwamiji salama na mahali pazuri

kwa kuishi na kufanya kazi.


Aidha, aliekeza wataalam wa mipangomiji

nchini kusimamia kikamilifu utekelezwaji wa mipango kabambe 

iliyoandaliwa katika maeneo yenu na mipangokina ili kuwa na 

uendelezaji wa mji unaozingatia mipangomiji.


" Ninyi wataalam wa 

mipangomiji mnapaswa kuwa na wivu na taaluma yenu na msiruhusu 

kuharibika kwa miji machoni mwenu," alisema waziri Mabula


Kwa upande wake Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema Wizara imejipanga kujikita mwenye Matumizi ya Tehama ambapo Wananchi Sasa wataanza kulipa Kodi ya pango la Ardhi kwa kupitia simu zao za mkonini Kama wanavyolipa Ankara za maji au Ankara zingine.


Amesema  kumekuwa na Changamoto kubwa kwa Wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi hivyo maelekezo ya waziri wetu Angelina Mabula wananchi wapelekewe huduma kwa kupitia simu zao za mkonini ili kuweza kulipa Kodi hiyo kwa wepesi na urahisi zaidi.


Pia Katibu Mkuu huyo amesema kupitia Matumizi hayo ya Tehama yatasaidia na kuboresha  makusanyo na mapato ndani ya wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi


"Hapa naomba nitoe msisitizo juu ya Matumizi ya Teknolojia Jambo litakalo saidia kuendana na Kasi ya kukuwa kwa miji na kuendana na idadi ya Watu , " amesema Mhandisi Sanga


Aidha amesema  kupitia mpango huo wa Matumizi ya Tehama itakwenda kusaidia kupinguza migogoro ya ardhi kwa Wananchi.



Mwenyekiti wa bodi ya usajili wa Wataalam wa Mipango miji John Lupala Amesemaa jukumu lamsingi la Bodi nikusajili wataalamu wa Mipango miji ambapo katika Kipindi chote Machi 2023 bodi imeweza kusajili 508 ambapo wataalam 36 wamefutiwa usajili kwasababu mbalimbali ukiukwaji wamaadili wa kitaalauma na kubakiwa na wataalamu 472.


Amesema bodi iliweza kusajili makampuni za Mipango miji 100 ambapo kampuni 13 Kutokana na sababu Mbali ziliweza kufutiwa usajili na kubakiwa na kampuni 87 zilizopo hadi sasa


Naye rais wa Chama Cha Wataalam wa Mipango miji Tanzania (TITP) Dkt Juma Matindana niukweli usiopingika muundo uliopo sasa kunamkanganyiko licha ya jitahidi za kuweka mambo sawa kwani wataalamu wapo Wizara na hata TAMISEMI kuwekwa sawa usiwe na ukakasi.


Aidha amesema wataalamu wa Mipango miji wa meshiriki kwa kiasi kikubwa Sana Serikali na binafsi wametumika katika kazi za urasimishaji ambapo mapaka Sasa kunamichoro ya Mipango miji vipande vilivyotambuliwa na kupangwa ni takriban Milioni 2400000.


Tukichukua ule wastani wa  kiwanja 150000  hii ni ile project ambayo ni bilioni 360 Lakini ripoti inaonyesha kubeti sio zaidi ya Bilioni 100 Yani 90 mpaka 100 ndio zimekusanywa kwa makampuni yalishirika katika upimaji na upangaji .


Aidha alisema Miradi hiyo imetoa Miradi mikubwa kwa vijana wanaomaliza katika vyuo vya ardhi ambapo Ilani ya Chama inasema hadi ifikapo 2025 wawe wametengeneza ajira zisizopungua Milioni 8 

Comments