ZAIDI YA WAKAZI 290,000 MJI WA USHIROMBO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA

 


Bukombe-Geita

wakazi 29,672 mji wa Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoani Geita wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na salama kupitia vyanzo vya maji hayo ni visima viwili virefu vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita 19,700 kwa saa na mradi hadi sasa umekamilika kwa asilimia 95.

Getruda Deogratius 
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Ushirombo 

Hayo yalielezwa na mkurugenzi mtendaji mamlaka ya maji Ushirombo Getruda Deogratius wakati wa mwenyeki wa CCM mkoa na viongozi wa serikali wakikaguwa miradi ya maendeleo kabla ya kuzindua sherehe za madhimisho ya miaka 46 kuzaliwa kwa CCM mkoa wa Geita.


Alisema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mamlaka ya maji Ushirombo kuna miradi ya maji inayo tekelezwa na wakandarasi wa miundombinu na usambazaji maji ambao ni AFIRICA ONER CO LTD na SALU & CO LTD.


Deogratius alisema mradi wa kwanza ni mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika mji wa Ushirombo inaotekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya AFIRICA ONER CO. L.T.D.


Alifafanua kuwa uboreshaji wa mradi wa maji Mjini Ushirombo inajengwa kwa mikataba mitatu mkandarasi wa ujenzi na mzabuni wa pampu na mwingine ni mzabuni wa bomba kwa gharama ya sh 859.3 milioni Mradi huo unatekeleza chini ya program ya mpango wa maendeleo ya ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa sh 591.5 milioni na malipo kulingana na matokeo ( PforR) kwa sh 336.6 milioni.

Martine Shigela (Katikati)

Mkuu Wa Mkoa Wa Geita


Akihutubia wanachama na wananchi katika viwanja vywa CCM wilaya ya Bukombe mkuu wa mkoa wa Geita Maritine Shigela alisema serikali ya awamu ya sita inaleta zaidi ya sh .1bilioni kila mwezi kwa ajili ya wanafunzi kwa kutekeleza agizo la serikali Elimu bure, mwalimu anae rudisha wanafunzi nyumbani anafanya makosa na sio maelekezo ya serikali hivyo nimarufuku kurudisha mwanafunzi kwa kukosa vifaa au michango hayo yanamhusu mzazi.


Martine Shigela alisema Desemba kuelekea Januari 2023 serikali ilileta Sh 12.8 bilioni zimejenga na kukamirisha vyumba 640 na fedha hizo zimewezesha kuazisha shule mpya zaidi ya 30.


Alisema wazazi na walezi wanapo kubaliana kuchagia nguvu zao na mali zao kwa kununua madawati kujenga vyoo wasihusishwe wanafunzi na mwalimu anae fukuza wanafunzi sio agizo la serikali ikiwa Rais Samia Suhulu Hassan hapendi kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani.

Nicholaus Kasendamila
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila akizindua sherehe za miaka 46 kuzaliwa kwa CCM aliunga mkono na kuogeza kuwa vitendo hivyo vya baadhi ya walimu vizibitiwe halaka ili wananchi waendele kuiamini serikali yao.


Kasendamila aliwaomba viongozi wa chama kuanzia ngazi ya tawi kuazisha ujenzi wa ofisi ya CCM kila tawi na kushirikiana na viongozi ngazi ya kata Kuazisha miradi ya kiuchumi ndani ya chama kwa kila kata.



Katibu wa CCM wilaya ya Bukombe Odilia Batimayo ameahidi kutekeleza maelekezo ya kiongozi wa chama mkoa ili chama kiwe na vyanzo vya mapato na kukuza uchumi.


MWISHO

Comments