WAZAZI WATAKIWA KUPELEKA WATOTO WENYE ULEMAVU SHULENI


  Wazazi na walezi wilaya ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kuwafichuwa na kuwapeleka watoto wenye ulemavu shuleni ili waweze kupata haki ya Elimu na kufikia malengo yao.

Hayo yamesemwa na afisa Elimu  Maalumu wilaya ya Bukombe Joyce Mangi wakati wa uzinduzi wa kuchimba msingi wa ujenzi wa mradi wa bweni la wanafunzi 80 wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Ushirombo.

Mangi alisema  wilaya ya Bukombe inawanafunzi wenye mahitaji maalumu 293 wenye ulemavu mbalimbali wakiwemo watu wenye Ualbino, viziwi, wasioona, na wenye ulemavu wa viungo  hata hivyo amesema bweni hilo likikamilika litaondoa changamoto kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wenye mahitaji malumu kupunguza gharama ya kuwaleta shule na kuwarudisha nyumbani watalazimika kukaa shuleni hapo.

Mkuu wa shule ya msingi Ushirombo Peter Jemes alisema shule imepokea sh 100 milioni kwa ajili ya ujenzi wa bweni bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu   katika kitengo maalumu  shuleni hapo ikiwa nimuhimu sana hivyo serikali na wadau wa Elimu wasichoke kutoa mali zao kwenye shule za wanafunzi wenye mahitaji malumu.

Mwenyekiti wa chama Cha watu wenye Ualbino (TAS) wilaya ya Bukombe Ida Saka amesema kutokana na shule hiyo kutokuwa na bweni kunabaadhi ya wazazi na walezi walikuwa wanashindwa kuwapeleka watoto wao shule wenye mahitaji malumu wanao ishinao majumbani hali ambayo ni kuwanyima haki zao za msingi  lakini kwa utekelezaji wa mradi huu utakapo kamilika bweni basi wataenda kupata haki yao ya msingi kikatiba.

Miongoni mwa wazazi wa wanafunzi Anatori Jonh ametoa wito kwa wazazi wezake wasiwafiche watoto wenye mahitaji malumu majumbani kwa kuachana nazana potofu ambayo imejengeka watoto hao hawawezi huku wanaweza.

Alisema zana potofu bado ipo ya kuficha watoto wenye ulemavu badala yake wawapeleke shule ili waweze kupata Elimu  kwa sababu  Serikali imetowa fedha ili wanafunzi wote waweze kupata elimu bira ubaguzi.

Naye mwanafunzi mwenye mahitaji malumu shule ya msingi Ushirombo Christina Samweli ameishukuru serikali kwa kuwaletea fedha za kujengea bweni litakalo wasaidia  kupunguza changamoto kwa baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaotoka mbali wengiwao hushindwa kutembea hadi shuleni kutokana na mahitaji yao huku wengine hughalimiwa na wazazi wao kwenda na kurudi nyumbani.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe  Lutengano Mwalwiba akizungumza kwaniaba ya mkuu wa wilaya katika uzinduzi huo wa ujenzi wa bweni amewaomba wazazi na walezi na wananchi kwa pamoja kuendela kuiunga mkono serikali kwa kujitolea nguvu zao katika miradi ya maendeleo ambayo inaletewa fedha na serikali.

Lutengano alisema ujenzi huo umeanza leo unatarajia kukamirika ndani yasiku 45 mwezi mmoja ma nusu kuanzia Februari 2023  hadi Aprili 5, 2023 hivyo wananchi waendele kushirikiana na viongozi wa serikali kuiunga kwa kuchimba msingi wa bweni la watu wenye mahitaji maalumu na umoja huo  unasaidia Sana kupunguza gharama ya mradi  na kuhakikisha mradi unakamilika kwa asilimia miamoja .


MWISHO

Comments